Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, January 13, 2016

Haya Ndiyo Mambo Unayolazimika Kuwa Na Mashaka Nayo Katika Maisha Yako.

No comments :
Ili kufanikiwa unatakiwa kujiamini na kutokuwa na wasiwasi na mambo mengine ambayo yanaweza kukuzuia kufanikiwa. Lakini pamoja na umuhimu huo wa kujiamini na kutokuwa na mashaka au wasiwasi wa kitu chochote lakini yapo mambo ambayo ni lazima uyawekee mashaka ili ufanikiwe.
Inapotokea mambo hayo ukayapokea jinsi yalivyo, bila kujiuliza au kuyawekea mashaka yoyote ni wazi utakuwa umejitengezea mazingira ya kushindwa wewe mwenyewe. Kwa kuweka mashaka hayo itakusaidia sana kusonga kwa kuchukua hatua mbadala.
Siku zote……..
Kuwa na mashaka hasa pale yanapotolewa majibu rahisi kwa tatizo ambalo ni kubwa. Lakini sio hivyo tu, likiwa ni tatizo ambalo linatakiwa kutolewa majibu ya uhakika. Hapo unatakiwa kuwa na mashaka kabisa na majibu hayo.
Kuwa na mashaka na watu ambao hawakubaliani na wewe. Badala ya wewe kujiona hufai kwa kutokubaliwa anza kuwatilia mashaka wao kwanza. Kwanini uwatilie mashaka? Kwa sababu wameshidwa kutamba thamani kubwa iliyo ndani mwako.
Kuwa na mashaka na njia zote ambao unaambiwa kwamba ukizitumia zitakupa utajiri wa haraka. Hizo njia ni za kuogopa na kukwepa sana. Kama njia hizo zipo, basi watu wengi wangekuwa matajiri sana. Hivyo, acha kuendelea kudanganywa kwa namna hiyo tena.

KUWA NA MASHAKA KWA KILE USICHOKIELEWA.
Kuwa na mashaka…
Kuwa na mashaka na wale watu wote wanaokwambia uwaamini. Uaminifu kwa jinsi ulivyo unakuja wenyewe kutokana na vitendo vyako. Lakini  sio jambo la kuambiwa kirahisi tu kwamba ‘niamni ‘ na ukajenga uaminifu mkubwa.
Pia siku zote kuwa na mashaka sana, kuishi maisha ambayo hayana mipango maalumu ya uhakika. Haya ni maisha mabaya sana si kwako tu, bali hata kwa wengine. Kwa yeyote anayeishi maisha haya ni vigumu sana kufikia mafanikio makubwa.
Kuwa na mashaka sana kama upo kwenye safari ya mafanikio ambayo haina makosa. Ukijiona upo kwenye safari hii, kwanza elewa kabisa inawezekana unafanya mambo madogo sana na kama si hivyo inawezekana huchukui hatua. Mafanikio wakati mwingine yanakuja kwa kukosea, kama hukosei kabisa unategemea nini?
Kuwa na mashaka…
Siku zote kuwa na mashaka na kile kipindi ambacho hasira inataka kukuendesha wewe. Unapokuwa na hasira halafu ukaona unaanza kuchukua maamuzi ya upesi, kuwa makini sana hali hiyo. Hicho ni kipindi unachotakiwa kuwa nacho makini sana, la sivyo utaharibu mengi.
Kuwa na mashaka na tabia ya kufuata kila wanachofanya wengine. Hii na tabia inayowapoteza wengi sana katika kufikia mafanikio makubwa. Badala ya mtu kufuata kile kilichopo kwenye malengo, wengi wanakuwa wanafuata watu wengine. Kama una tabia hii kuwa na mashaka nayo sana.
Kuwa na mashaka na wale wanaofanya kazi kidogo na kutegemea kupata matokeo makubwa. Hawa ni watu wa kuwa nao makini sana siku zote za maisha yako. Ili uweze kufanikiwa unahitaji kufanya kazi haswaa, ila kama utafanya kidogo na kutegemea makubwa hapo kuna mashaka tena.
Kuwa na mashaka…
Kuwa na mashaka sana na watu wote wale wanaotegemea mambo mazuri yatakuwa kesho na hakuna mipango inayowekwa. Hawa ni watu hatari sana. kila siku, kila mwaka wataongea hivyo, lakini hakuna utendaji wa maana unaotokea. Kuwa na mashaka sana na watu hawa.
Kuwa na mashaka na jambo ambalo ukitaka kulifanya ukaliweza moja kwa moja. Jambo ambalo linaweza kukupa mafanikio makubwa ni lile ambalo linaweza likakupa changamoto kubwa na nzito katika maisha yako. Mambo mepesi hayawezi kukutoa kwenye umaskini.
Kuwa na mashaka na watu wote wanaokata tamaa na kuamua kuzika ndoto zao mapema. Hawa ni watu hatari sana kwako ambao unatakiwa kuwaogopa. Kitendo cha kuwa na watu hawa ni rahisi kukufanya hata wewe usiweze kufanikiwa. Kuwa na mashaka nao.
Kuwa na mashaka…inaweza ikawa ni njia bora ya kukusaidia kuboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment