Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, January 26, 2016

Tabia 5 Unazotakiwa Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.

No comments :
Ili kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa tajiri ni safari inayohitaji kujituma na uwe mvumilivu hadi kufikia mafanikio hayo. Wengi hujikuta kushindwa kufikia mwisho wa safari hii kwa sababu mbalimbali zinazowakabili. Lakini moja ya sababu hizo ni tabia mbaya wanazokuwa nazo hasa pale wanapokuwa na pesa.
Unaweza ukashangaa kwa nini naziita tabia mbaya? Usipate tabu, hizi ni tabia mbaya kwa sababu ndizo zinazowakwamisha na kuwarudisha wengi nyuma kimafanikio zaidi. Sasa wengi wanakuwa ni watu wa kushikiria tabia hizi ambazo wanatakiwa kuziacha mara moja. Kwa kung’ang’ania huko huwarudisha nyuma sana kimafanikio.
Je, unajua ni tabia zipi unazotakiwa kuziacha mara moja hasa pale unapokuwa na Pesa?
Zifuatazo Ni Tabia 5 Unazotakiwa Kuziacha Mara Moja Unapokuwa Na Pesa.
 1. Kutokupangilia matumizi.
Ili uweze kufanikiwa na kutunza pesa ulizonazo ni vyema sana ikiwa utapangalia matumizi yako kila siku. Unapokuwa unapangilia matumizi yako inakuwa inakusaidia sana kutokutumia pesa zako hovyo. Ni rahisi sana kutumia pesa zako hovyo kama hujaandika popote. Kutokupangilia matumizi ni moja ya tabia unayotakiwa kuiacha mara moja ili kufanikiwa.

PANGILIA MATUMIZI YAKO VIZURI.
2. Kutumia kila pesa unayoipata.
Mara nyingi watu walio wengi hutumia pesa zao zote walizonazo bila ya kuweka akiba hata tone. Haya ni maisha ambayo wengi wamekuwa nayo na wanayaishi kila siku. Kila wanapoulizwa kwa nini iko hivyo, sababu yao ni moja tu kwamba pesa haiwekekiki. Na kwa imani hiyo hujikuta hakuna akiba wanayoiweka na kubaki kuishi maisha magumu. Kama nia yako kubwa ni kufanikiwa achana na tabia hii mara moja.
3. Kufanya matumizi yasiyo ya lazima.
Kuna watu wanapokuwa na pesa huwa zinawasumbua sana. huwa ni watu wasiotulia kwa kutaka kununua karibu kila kitu wanachokiona mbele yao. Unapokuwa na tabia hii kwa uhakika unakuwa sio rahisi kuweza kufanikiwa. Kitu ambacho kinakuwa kinakufanya ushindwe kufanikiwa ni kwa sababu pesa zote unakuwa unazitumia hovyo na kushindwa kuweka hata akiba ya kukusaidia
4. Kutokuweza.
Utakuwa upo kwenye hatari sana kwenye maisha haya kama utakuwa unaishi maisha bila ya kuwekeza. Kuwekeza ni jambo la msingi sana ambalo unatakiwa ulitilie mkazo kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi. Ili uweze kufanikiwa unalazimika kuwekeza pesa zako na sio suala kutumia tu. Kutokuwekeza ni moja ya tabia unayoitakiwa kuicha ili kujenga mafanikio ya kudumu.
5. Kushindwa kulipa madeni yako mapema.
Yapo madeni ambayo wengi hutakiwa kulipa mapema, lakini hata hivyo wengi pia hujikuta wanashindwa kulipa madeni hayo kwa muda mwafaka. Kitu cha msingi hapa kama kuna madeni unadaiwa kwa mfano ada za watoto, kodi mbalimbali ni vyema ukalipia mapema na kwa utaratibu ili kujiepusha na usumbufu ambao unaweza ukjitokeza kwako kwa baadae.
Kama utachukua hatua na kuamua kuachana na tabia hizo utajijengea mazingira ya kufikia mafanikio makubwa kwako kwa kadri siku zinavyokwenda kwenye maisha yako.
Nakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe upande wako. Kumbuka endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu, 
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment