Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, January 11, 2016

Mambo Matatu Ya Lazima Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.

No comments :
Kila mtu ana malengo yake ambayo anakuwa anajiwekea mara kwa mara katika maisha yake. Wengi kati yetu tumekuwa ni watu wa kujiwekea malengo siku hadi siku, bila shaka hili halina ubishi. Wapo ambao hujiwekea malengo madogo na wengine kujiwekea malengo makubwa. Kwa hiyo utaona kila mtu ana malengo ya aina fulani ambayo amejiwekea.
Lakini pamoja na kujiwekea malengo hayo, kitu cha kushangaza kwa wengi wamekuwa ni watu wa kushindwa kufikia yale malengo yao. Najua umeshawahi kuona watu ambao hawafanikiwi kwa sababu ya kushindwa  kuyafikia malengo yao. Kitu cha kujiuliza ni kwa nini wengine waweze kufikia malengo yao na wengine washindwe?
Je, kwa wale wanaoshindwa kufanikiwa, malengo yao huwa ni magumu sana kuyafikia au hayawezekani kabisa au kuna sababu nje na hapo?Ni jambo unalotakiwa kulijua na kulifanyia kazi ili na wewe usiingie kwenye mtego wa kushindwa kufikia malengo yako mara kwa mara.
Kwa wengi wanaoshindwa, mbali na kukosa mipango na malengo au kuchukua hatua, kitu kingine kinachowafanya washindwe kufikia malengo yao ni kule kushindwa kujua mambo ya lazima wanayotakiwa kuwa nayo wakati wanajiwekea malengo. Ukiyajua mambo hayo ni njia ya uhakika kufikia malengo yako yoyote uliyojiwekea.
Yafuatayo Ni Mambo Matatu Ya Lazima Yatakayokusaidia Kufikia Malengo Yako.
1. Jijengee mawazo chanya.
Muda wote wakati umejiwekea malengo yako ni muhimu sana kuwa na mawazo chanya. Acha kuwaza kwamba utashindwa, jenga picha ya mafanikio unayoyataka ikiwa utatimiza malengo yako. Kwa kufaya hivyo itakujengea kujiamini sana na mwisho wa siku utatimiza malengo yako. Hili ni jambo la lazima sana kwako unalotakiwa ulijue ili kufikia malengo yako.

KUWA NA MAWAZO CHANYA MUDA WOTE.
2. Fanyia kazi mabadiliko yote.
Wakati unaweka malengo yako ulijipa ahadi na kupanga kabisa utaachana na mawazo hasi, hutafikiri kushindwa na utajituma. Kama hicho ndicho ulichojiahidi endelea kukifanyia kazi bila kuchoka. Fanya mabadiliko yote ya muhimu na yaweke kwenye utekelezaji mara moja bila kuacha kitu. Hiyo itakusaidia sana kufikia malengo yako makubwa.
3. Endelea kufanyia kazi mabadliko.
Kwa kawaida tunapoweka malengo kuna chanagamoto na mambo mengi tunayokutana nayo. Changamoto hizo na mabadiliko yoyote endelea kuyafanyia kazi siku zote bila kuchoka. Kama ni kuwa na mawazo chanya endelea nayo. Kama ni kufikiri ushindi endelea hivyo hivyo mpaka mafanikio yatokee upande wako.
Kwa jinsi utakavyozidi kutumia njia hizo, ndivyo malengo yako yatazidi kutimia kwa uhakika mkubwa.
Nikutakie siku njema iwe na mafanikio makubwa sana.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
No comments :

Post a Comment