Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, January 21, 2016

Mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.

No comments :
Sasa baada ya utafiti wa muda mrefu imegundulika kwamba macho yetu yana uwezo wa kutufundisha mengi sana ikiwa tutakuwa tunayachunguza kwa umakini. Wataalamu hao wamegundua macho yetu yana uwezo wa kutuonyesha mambo mbalimbali  kama tunasema uongo au ukweli,  kutuonyesha jinsi tunavyofikiri na hata kutoa mustakabali wa afya zetu.
Kwa  mujibu wa wataalamu hawa wanadai kwamba yapo mambo mengi yaliyofichika kwenye macho yetu bila hata sisi wenyewe kuelewa. Hii ni sayansi ambayo inaweza ikawa ya kustaabisha kidogo kwako, ingawa ukweli wa mambo ndivyo ulivyo na utabaki hivyo. Ni vyema sana kama ukafahamu vizuri mambo yaliyofichika kwenye macho yako.
Yafutayo Ni mambo Matano Yaliyofichika Kwenye Macho Yako.
1. Magonjwa uliyonayo.
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika zinaonyesha kwamba rangi za macho yetu zinauhusiano mkubwa wa moja kwa moja na baadhi ya magonjwa yanayotupata. Kwa mfano watu wengi wenye macho yanayoonyesha rangi ya ‘bluu’ hawa hupatwa sana na magonjwa ya kisukari, mabaka mabaka mwilini na kansa ya ngozi.
Lakini hata hivyo kuna wengine wanakuwa wana macho yana rangi za aina mbili kwa mfano labda ‘bluu’ na ‘brown’. Kwa watu kama hawa magonjwa yanayowakumba ni kama vile ngozi kukakamaa maeneo ya usoni. Kwa hali hiyo ukichunguza watu wenye macho ya rangi ya ‘bluu’ wengi wanasumbuliwa sana na magonjwa hayo.

MACHO RANGI YA 'BLUU'
2. Haiba yako.
Macho yako pia yana uwezo mkubwa wa kuonyesha haiba uliyonayo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Australia na  jopo la waataalamu lililoshirikisha watu 366,  utafiti huo unaonyesha kwamba watu wenye macho hasa ya mng’ao (bright eyes) mara nyingi hawa wana mvuto mkubwa sana kwa jamii ikiwa ni pamoja na kwenye masuala ya kimapenzi.
Na wakati huo watu wenye macho meusi (dark eyes) utafiti huu unaonyesha hawa ni watu ambao hawana mvuto sana katika jamii, mara nyingi huwa ni wa kimya na mambo yao kwa ujumla usipowachunguza hata kidogo huwa yanayoonekana ni kama vile hayaeleweki na ni ngumu kuwatambua kirahisi.

UGONJWA WA MABAKA MABAKA (VITILIGO)
3. Maumivu unayobeba.
Pia utafiti unaonyesha macho yana uwezo wa kuonyesha kwamba wewe ni mtu mwenye uwezo wa kubeba maumivu ya aina gani. Kwa mfano wanawake wenye macho ya mng’ao (bright eyes) utafiti unawaonyesha kwamba hawa hupata maumivu kidogo pale wanapojifungua tofati na wanawake wenye macho ya ‘dark blue’.
Wanawake hawa wenye macho ya mng’ao ( bright eyes)  si tu kwamba wanakuwa wana maumivu madogo wakati wanajifungua lakini pia ni watu wenye hofu kiasi, hawana msongo wa mawazo mkubwa na pia si watu wa kuwaza hasi sana. Pia hiyo haitoshi inapotokea wakanywa pombe kwao huwa sio rahisi sana kulewa.

MACHO RANGI YA 'BROWN'
4. Maumbile yako.
Ni ukweli ulio halisi pia macho yako yana uwezo wa kututambulisha maumbile (Genetics) ulizonazo. Kwa mfano mwaka 2008 wanasayansi waliweza kugundua kwamba watu wote wenye macho ya ‘bluu’ wamerithi maumbile au genetics moja kwa moja kutoka kwa baba zao. Kwa hiyo ni watu wanaofanana na baba zao.
Pia si hivyo tu, watu hawa wenye macho ya ‘bluu’ wamerithi pia mambo mengi kutoka kwa babu zao. Wana vitu vinavyofanana na babu zao na pia kutoka kwa baba zao. Kwa msingi huo utagundua watu hawa wenye macho ya ‘bluu’ mambo mengi warithi sana kutoka kwa baba au babu zao. 

MACHO RANGI YA MNG'AO (BRIGHT EYES)
5. Namna gani unavyoaminika.
Macho ulionayo yana uwezo wa kutuonyesha jinsi unavyoamika. Utafiti unaoyesha watu wengi wenye macho ya ‘brown’ ni watu wa kuaminika sana katika jamii kuliko watu wenye macho tofauti na hayo.
Hivyo basi, macho yako yanauwezo wa kubeba haiba, maumbile, uaminifu, maumivu na hata magonjwa. Hayo ndiyo mambo yanakuwa yamefichka mara kwa mara kwenye macho yetu.
Nikutakie siku njema sana na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki katika mafanikio, 
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment