google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 12, 2021

Siri Ya Ndani Ya Mafanikio.

No comments :

 

Kuna wakati tunapowaangalia watu wenye mafanikio, huwa tunafikiri kwamba, wana siri za ndani sana ambazo wanazo na ndio zimewafikisha hapo walipo kimafanikio. Mawazo kama hayo huwa yapo sana ndani mwetu.

Kitu usichokijua watu hao huwa hawana siri ya ndani kubwa kivilee ambayo  imewafikisha unapowaona. Jambo kubwa kwao linalowabeba na  kuwafanya wafanikiwe ni kupitia kufanya na kufanya. 

Kwa jinsi wanavyoendelea kufanya, watu hao hujifunza vitu vingi sana, na ambavyo huvifanyia kazi kila siku na mwisho wa siku hujikuta wamebobea kiasi cha kwamba huonekana wana siri kubwa sana.

Kwa chochote kile unachokifanya, ukiamua kukifanya huku ukawa unajifunza, na kuhakikishia utakifanya vizuri sana, na kugundua mambo mengi yaletayo matokeo bora. 

Kwa kuwa umeamua kufanya kazi huku ukijifunza, utafanikiwa. Watu wengine wakikuona watajua, naamu jamaa ana siri ya pekee, kumbe kupitia kufanya na kufanya tena unajifunza yote hayo.

Akili yako na mwili wako, vina uwezo mkubwa sana wa kuweza kudaka kile unachojifunza. Hivyo ukijifunza chochote utaweza, na watu wataona una siri za pekee za mafanikio yako, kumbe wewe umezipata kwenye kupitia kufanya.

Kwa kuwa umeshajua hakuna siri ya pekee na ya ndani, yote unayoyaita siri utayapata kupitia kufanya na kufanya tena, hivyo amua kuchapa kazi huku ukijifunza, ni hivyo tu na ni rahisi.

Watu wengi wanafanya wanayoyafanya pasipo kuamua kujifunza. Ndio maana utakuta watu hao wapo pale pale miaka nenda, miaka rudi, sababu kubwa ni hawajifunzi.

Kama unafanya na hujifunzi, basi kila utakapowaona watu wenye mafanikio, hutasita kuwaona wana siri kubwa, pia huta sita kuwaona ni watu ambao kama ni wachawi au wamefanya vitu vibaya ili kufanikiwa.

Narudia, fanya kazi zako huku ukiamua kujifunza kweli. Andaa daftari la kujifunza yale yanayotokana na kazi yako. Jifunze yote mabaya na mazuri na yatakuwa ngazi kwako ya kukupa hizo unazoziita siri za ndani, kumbe hata hizo siri hazipo.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.