google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 6, 2021

Ubora Na Mambo Makubwa Vinakuja Hivi...

No comments :

 


Hakuna ubora ambao unaweza ukaupata, kama tu ndio unafanya kwa mara ya kwanza. Ubora unatakiwa kutengenezwa kwa wewe kuamua kufanya tena na tena, bila kuchoka.

Hakuna mambo makubwa ambayo unaweza ukayapata tu kwa wewe kufanya kwa mara ya kwanza. Mambo yote makubwa yanakuja kwa wewe kufanya tena na tena, na kwa kujituma.

Unachotakiwa kufanya, ni kuanza. Anza hatua ya kwanza ya kuelekea ndoto zako. Usiwaze kwanza utafanya kwa ubora mkubwa kiasi gani. Waza namna utakavyoanza. 

Yapo mambo mengi sana ambayo utajifunza ikiwa utaanza tu. Ikiwa hautaanza na kutaka kufanya kwa ubora tu, basi unajidanganya na utajikuta hutafanya kitu na hata huo ubora utaukosa.

Unaweza ukawa umefanya makosa, jifunze na songa mbele. Unaweza ukawa umekatishwa tamaa, hiyo sio hoja, songa mbele.  Unaweza ukakutana na kila aina ya ugumu, hilo bado si tatizo kwako.

Kitu cha msingi kwako ni kusonga mbele na kukamilisha kile ulichotakiwa kukifanya tena kwa uhakika. Usitake makubwa mwanzoni, usitake ubora sana mwanzoni, fanya kwanza.

Kaa ukijua ubora na mambo makubwa, haviji mwanzoni, hivyo vinakuja mpaka wewe uwe tayari umeshachukua hatua za kufanya, hata ukikosea wewe fanya tu hadi ufanikiwe kwa mafanikio makubwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.