google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 18, 2021

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuipa Akili Yako Ushawishi Na Ikupe Mafanikio.

No comments :

Wataalamu wengi wa mafanikio wanasisitiza sana umuhimu wa kupitia malengo yako kila siku ili iwe rahisi kwako kuweza kuyatimiza. Unajua ni kwa nini hili linasisitizwa sana? Umeshawahi kujiuliza kwa nini?

Hiyo yote ni kuufanya ubongo wako uamini kwamba malengo yako yanawezekana. Hiyo iko hivyo pia kwa sababu kabla hujafikisha miaka mitano unakuwa umekataliwa mara 40,000 kwa vitu tofauti na ni mara 5000 tu ndio unakuwa umekubaliwa.

Mpaka hapo unaona kama umekataliwa mara nyingi hivyo, tafsiri yake ni rahisi kuona kila kitu hakiwezekani. Ili mambo hayo yawezekane sasa, inabidi uushawishi ubongo wako kuamini kwamba inawezekana. 

Kumbuka mafanikio yanaanza na sisi wenyewe kwanza, yaani zile imani tulizonazo ndani mwetu, ndizo zinajenga mafanikio. Hivyo unatakiwa kujilisha vitu chanya na kujiaminisha kwamba inawezekana kwa lolote lile kwako, pitia malengo yako kila siku utafanikiwa.

Hakuna namna utakayoweza kuifanya akili yako iamini kuwa utafanikiwa zaidi ya kuandika malengo yako na kuyapitia kila siku. Ukifanya zoezi hilo kila siku la kuyapitia malengo yako, utaipa akili yako ushawishi mkubwa sana na utafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.