google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 15, 2021

Acha Mazoea Haya Ili Ufanikiwe.

No comments :

 

Ili kuweza kwenda mbele kimaisha kwa uhakika na kikamilifu, unatakiwa kuna baadhi ya mazoea ya kila siku kuyaacha na kuyasahau maishani mwako.

Kama ukiendeleza mazoea unayoenda nayo kila siku, huwezi kufika mbali sana, utakwama. Mazoea uliyonayo yanaweza kukukwamisha na kukufanya ushindwe kupiga hatua.

Kwa mfano, yapo ambayo kuna watu wanayo ya kufanya kazi moja kwa moja pasipo kujipa mapumziko ya muda. Kujipa mapumziko au rikizo ni muhimu hata kama hujaajiriwa na mtu.

Hata iweje, huwezi kufanya kazi moja kwa moja kama katapila bila mapumziko yoyote yale. Mapumziko ni muhimu sana kwako kwa sababu yatakusaidia kuja na kasi kubwa.

Angalia, hata miti huwa haikui moja kwa moja, kuna kipindi ambacho inapukutisha majani, na kuna kipindi inatengeneza majani upya. Iko hivyo ili kupata kasi ya ukuaji mzuri.

Maisha pia ni matokeo ya juhudi na kupumzika. Uhodari wa kimoja, unategemea kingine. Ukiweka nguvu zako nyingi katika kazi, basi utakuwa una muda mzuri pia wa kuweza kupumzika. 

Kuendelea kufanya kazi kwa mfululizo, pasipo kujipa muda wa kupumzika, kaa ukijua kuna ubora utaupunguza. Kazi hiyo haiwezi kuwa bora kama ilivyotakiwa iwe.

Ukipiga kazi kwa nguvu, jipe muda wa kujipumzisha, na hapo utaifanya akili yako ifanye kazi kwa ufasaha sana na kukupa matokeo makubwa katika maisha yako na yenye maana.

Acha kuishi kwa mazoea, acha kuishi kwa kujinyima mapumziko, chapa kazi zako na huku usisahau kujipa mapumziko ambayo yatakupa tija na mafanikio makubwa .

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.