google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 16, 2021

Jambo La Kufanya, Kama Hupati Matokeo Unayoyataka.

No comments :

 

Ikiwa unapata matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge, hujiwezi na kukata tamaa, endelea kuweka juhudi tena na tena. 

Ikiwa unapitia kwenye changamoto nyingi za kimaisha, zinazokunyima matokeo, pia acha kukata tamaa, endelea kuweka juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto hizo na kuwa huru.

Ikiwa huridhiki kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye umepoteza, narudia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi, matokeo bora yatakuja.

Kwa kila hatua unayochukua kwenye maisha yako, inaleta mabadiliko haijalishi upo kwenye hali ya kukata tamaa namna gani.

Angalia ulikotoka kwemye maisha, sasa kwa nini ukate tamaa na wakati sasa hivi upo mbali sana? Dawa si kukata tamaa, bali dawa ni kuweka juhudi tena kwa kiasi kikubwa. 

Hata upate matokeo mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani lazima juhudi zako zitaleta matunda.

Hakuna mtu katika dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo hayupo.

Hivyo, hata ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa  huyaoni.

Kila hatua unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. Jambo la kufanya unapohisi umekata tamaa, ni kuongeza juhudi, ukiongeza juhudi utafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.