google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 19, 2021

Hii Isiwe Sababu Ya kukuzuia Kufanikiwa...

No comments :

Kuna watu hawafanikiwi kwa sababu, wanafanya kazi zao nusu nusu na zinaishia kati, hawafiki mwisho kule wanakotakiwa kufika. Watu kama hawa kufanikiwa ni ngumu.

Kwa mfano, ilitakiwa watu hao wafanye kazi zao zianze kuwalipa, kwa sababu hawafiki mwisho yaani wanaishia kati, basi hujikuta wafikii yale mafanikio yanayotakiwa.

Utakuta mtu ni mwimbaji mzuri sana, lakini hafanikiwi, kwa sababu, hajaweza kurekodi, hafanikiwi kwa sababu hajaweza kujiweka wazi akajulikana na kusaidiwa na watu wengine. 

Pia utakuta mtu ni mwandishi mzuri sana, lakini anakuwa hafanikiwi kwa sababu, mtu huyo anakuwa bado hajachapa kazi zake zikaonekana, hivyo kazi zake zinakuwa ni nusu hazijafika mwisho wa kumpa faida.

Wapo watu wa aina hii wengi, utakuta wengine wanafanya kilimo, lakini hawaweki ule ubora unaotakiwa ili wafanikiwe. Kwa kuishia kwao kati inaleta shida sana kwao na kuwazuia kufanikiwa.

Ili kufanikiwa kwa chochote kile unachokifanya, unatakiwa kufanya kitu hicho mpaka mwisho. Hutakiwi kuishia katikati, utakuwa unajipoteza wewe kwa kupoteza muda na nguvu zako bure.

Kwa chochote ukifanyacho, kifanye hadi mwisho na ukione kinakupa  mafanikio makubwa. Hapo ndipo ilipo siri ya mafanikio yako, yaani kufika mwisho. Kama hufiki mwisho, itakuwa kazi sana kwako kufanikiwa.

Kufanya kazi nusu nusu na kushindwa kufika mwisho isiwe hata sababu ya kukuzuia kufanikiwa. Kwa chochote ukifanyacho, nenda mazima mazima, hakuna kufanya kazi nusu nusu, hutafanikiwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.