google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 14, 2021

Weka Nguvu Zako Hivi, Kwa Chochote Ukifanyacho.

No comments :

  

Kama kuna kazi umeamua kuifanya, iwe biashara, kilimo, masomo au kitu chochote, basi,  ifanye kazi hiyo, kwa kuamua kuweka juhudi zako zote hapo bila kuacha kitu.

Usijaribu hata kidogo kuifanya kazi yako hiyo kwa kuweka nguvu zako nusu nusu, maana utapoteza muda wako na nguvu zako bure, na pia hutapata matokeo kama utakavyo.

Ili kuepuka kutopoteza muda wako, nguvu zako na hata kurudia kazi hiyo, dawa ni moja tu kuweka nguvu zako zote hapo na bila kupepesa macho, kwa kitu hicho ukifanyacho. 

Hebu jiulize, kwa nini kupoteza nguvu zako, muda, na kurudia kazi ambayo ulitakiwa kuifanya mara moja tu?  Kama nilivyosema ili yote hayo yasitokee, weka nguvu zako zote hapo.

Kumbuka unatumia muda wako wa thamani na nguvu zako pia. Unahitaji kutengeneza thamani sawa sawa na muda na nguvu zako unazotoa. Achana na kufanya mambo nusu nusu. 

Kubali kwa unachokifanya, kuwekeza nguvu zako zote. Ukiweka nguvu zako zote, nakwambia uwe na uhakika utaweza kufanikiwa na hakuna kitakachoshindikana kwako.

Kama ukiwekeza nguvu zako kwa unachokifanya, hata ikitokea umeshindwa, hutajilaumu kwa maana, ulifanya kila linalowezekana, ili uweze kufanikiwa na pia utajifunza. 

Kila wakati jikumbushe kwa chochote unachokifanya wekeza nguvu zako zote hapo. Kama huwezi kuwekeza nguvu zako zote ni bora kukiacha kitu hicho, maana hutafanikiwa sana.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.