google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 7, 2021

Jitangaze Wewe Kwa Kuwa Hivi...

No comments :

 

Ipo njia rahisi ambayo wewe, unaweza ukajitangaza, na kila mtu akawa na mvuto au akavutiwa na wewe na ukajikuta hata biashara yako unaifanya kiurahisi.

Njia hii sio nyingine bali ni ya kuvaa vizuri na kutembea vizuri. Mavazi yako na mwonekano wako ni ishara tosha ya kwamba wewe ni nani, na unafaa au hufai.

Hutakiwi kusahau kuwa kila siku na kila unapokuwepo unajitangaza wewe mwenyewe, kwa hiyo vaa vizuri, kuwa msafi na tembea kwa mwendo wa heshima. 

Kumbuka mtu anapokutana na wewe kwa mara ya kwanza anajitengenezea  picha yako kwenye akili yake ndani ya sekunde tano za mwanzo. 

Hakikisha picha hii ni nzuri na itakayokuletea fursa nyingi zaidi. Hakikisha mtu atakayekuona kwa mara ya kwanza akukubali wewe kwa jinsi ulivyo.

Acha kuvaa hovyo, wala kutembea hovyo, mwonekano wako ni matangazo tosha yanayokuonyesha wewe jinsi ulivyo,  linda mwonekano huo.

 Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.