google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 11, 2021

Kitu Kitakachokupa Ushindi Wa Mafanikio Yako Ni Hiki.

No comments :

 

Kitu pekee kinachokupa ushindi wa mafanikio ni juhudi zako za ziada. Kama huweki juhudi za ziada, kaa ukijua mafanikio huwezi kuyapata, mafanikio yanakuja kwa hatua za ziada tu.

Watu wanaofanikiwa na ambao hawafanikiwi huwa hawana tofauti kubwa sana. Kinachokuja kuwatofautisha ni zile juhudi zao za ziada. Wanaofanikiwa kila wakifanyacho wanaongeza juhudi za ziada.

Watu hao kwa kuongeza juhudi hizo za ziada, hujikuta ndio wanakuwa kwenye njia ya kutengeneza mafanikio yao, na kuwaacha wengine wakishangaa. 

Kila ukiwaangalia waliofanikiwa,utagundua ni watu ambao wao wanaweka sana juhudi za ziada tofauti na ambao hawajafanikiwa, ingawa tofauti ni kidogo sana.

Hivyo kila mafanikio unayoyaona, ni matokeo ya juhudi za ziada zilizoongezeka, ndio yakazaliwa mafanikio uyaonayo. Kila ilipoongezeka hatua au juhudi za ziada basi, zilileta mafanikio.

Juhudi inayoongeza kwa saa moja kila siku, hiyo pekee ndio inayokufanya uende mbele na si kurudi nyuma. Juhudi hiyo ndio inayokupa hasara au faida uliyokuwa ukiiwaza. 

Mafanikio yanajengwa, na hayatokei kirahisi na kwa bahati mbaya. Mafanikio yako yanajengwa kwa juhudi zako za ziada, yaani kwenda 'extra mile' kwa chochote ukifanyacho.

Juhudi unazoweka leo, ni msingi mkubwa wa mafanikio ya kesho.

Kila siku ukiwa mtu wa kuongeza juhudi, basi utakuwa unajitengenezea mafanikio makubwa sana.

Angalia wana riadha, wanashinda kwa sababu ya juhudi kidogo za ziada wanazoziweka na kuna kuwa hakuna tofauti kubwa sana na wale walioshindwa.

Hata wewe ukitaka kufanikiwa sana, weka juhudi za ziada. Kama hutaweka juhudi za ziada mafanikio kwako yatabaki historia na huwezi kufanikiwa kwa viwango vikubwa, utaishia kuwa mtu wa chini na kawaida kabisa.

Tatizo la watu wengi, wana mazoea ya kufanya kazi zao si kwa kwenda hatua ya ziada. Wanafanya kwa namna ile ile na wakiamini watafanikiwa. Usiwe kama wao, BADILIKA na utaona Matokeo makubwa.

Kila la kheri katika kufikia mafanikio yako.

Kama unapenda kujiunga na kundi la mafanikio ili uweze kujifunza zaidi mambo mengi ya kimafanikio. Tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 na utapewa utaratibu wa kuunganishwa.

Hakimiliki©2021 Imani Ngwangwalu. Haki Zote Zimehifadhiwa. Makala hizi hutolewa kwa ajili ya kuboresha maisha yako. Ruksa 'kushare' na usibadili kitu chochote bila ya ruhusa ya mwandishi.

 

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.