google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 1, 2021

Sheria Nne (4) Za Kujenga Utajiri, Hata Kama Huna Kitu Kabisa.

No comments :
Kwa kiasi kikubwa idadi ya tulio wengi bila  ya kujali ni maskini au tajiri  tumezaliwa katika familia maskini. Hata unapoona wengine wanakuwa wamefanikiwa sana, hiyo haina maana kwamba wao wametakotea katika koo au familia za kifalme, bali ni matokeo ya nguvu na juhudi zao wenyewe.
Kwa mantiki hiyo inamaanisha hivi, ili uweze kupata utajiri, mbali na juhudi binafsi zipo sheria ambazo mtu anatakiwa azifuate ili kufikia lengo hilo. Na kwa kufuata sheria hizo haitajalisha wewe umetokea katika familia gani au umetokea katika nchi au wewe ni wa rangi ipi ni lazima utafanikiwa.
Kwa kusoma makala haya ya leo, utajifunza sheria chache za msingi ambazo mtu unatakiwa uwe nazo au uzifahamu ili zikusaidie kujenga utajiri hata kama umetokea familia maskini. Uwezo wa kufikia utajiri unao tena sana, ni suala la kuamua na kuanza kutekeleza sheria za mafanikio. Sheria hizo ni zipi? Twende pamoja katika somo.

1. Tengeneza tabia za kukuwezesha kuwa tajiri.
Utajiri haujengwi kwa bahati mbaya hata kidogo. Zipo tabia ambazo unatakiwa uzijenge ili zikusaidie kutengeza msingi imara wa utajiri unaotaka kwenye maisha yako. Tabia ya kujiwekea akiba,  kutunza muda na kujenga maamuzi sahihi ya kimafanikio ni moja ya tabia bora ambazo ukiziendeleza kwa muda zinakupa mafanikio ya wazi.
Angalia sana katika maisha yako usije ukajuta kwa sababu ya tabia zako mbaya ambazo zitakuangusha  na kukufanya ukashindwa kufikia utajiri. Kuwa makini na tabia hizo, jikague na jenga tabia za kukuwezesha kufanikiwa. Kwa kadri unavyojenga tabia hizi kila siku, ndivyo utazidi kukaribia mafanikio yako kwa sehemu kubwa.

2. Fanya kazi kwa juhudi sana.
Ikiwa ndio unaanzia chini kabisa huna kitu, hakuna kitakachoweza kukutoa hapo ulipo zaidi ya kufanya kazi kwa juhudi sana. Hapa inabidi ufanye kazi kwa bidii tena huku ukiwa na nidhamu ya hali ya juu kwa kuhakikisha kila ukipatacho unakitunza vyema na kinakusaidia kufanikiwa kwako.
Kama umeamua kujitoa kisawasawa na kufanya kazi kweli na kuachana na maneno, utafanikiwa. Hii ni sheria inayotumiwa na watu karibu wote wenye mafanikio makubwa duniani. Siku zote watu hao ni wa kufanya kazi kwa bidii kubwa hali inayopelekea kuleta mafanikio yao ya uhakika na kujenga utajiri.
3. Tengeneza vyanzo vingi vya fedha.
Hakuna utajiri unaojengwa kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa, utajiri unajengwa kwa kujiwekea vyanzo vingi vya pesa. Kama una chanzo kimoja cha pesa na una nia ya kuwa tajiri hauataweza kuwa hivyo. Siri au sheria ya kuwa tajiri inakutaka wewe kutengeneza vyanzo vingi vya pesa.
Vyanzo hivyo vya pesa vitaingiza pesa bila kujali sana wewe unafanya kazi moja kwa moja au haufanyi. Matajiri wengi ndivyo wanavyotengeneza utajiri wao na hii ni siri mojawapo ambayo unatakiwa uijue kwa ufasaha. Huhitaji sasa kusita sita , weka vyanzo vingi vya pesa utengeneze utajiri wako.
4. Tambua namna ya kutunza pesa zako.
Itakuwa ni kazi bure kama unatafuta pesa,  hujui namna ya kuzitunza vizuri. Kuna watu ambao tatizo sio namna ya kupata pesa, bali ni jinsi ya kuzitunza pesa hizo. Utakuta mtu anapata pesa kweli, lakini matumizi yake yapo juu sana, hicho ni kitu ambacho ni sumu au kiziuzi cha mafanikio yake moja kwa moja.
Inabidi ufike mahali uwe na nidhamu ya hali ya juu, juu ya pesa zako, achana na matumizi ya hovyo, hayawezi kukufikisha popote. Kila wakati kaa chini na elewa namna ya kujifunza juu ya kutumia pesa zako kwa busara. Pesa zako zisije zikakufanya ukawa kama mwendawazimu, tulia ili ujenge utajiri wako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Nikutakie siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.