Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, March 2, 2017

Elimu Mahususi Katika Kukua Kwa Biashara Yako.

No comments :
Tumekuwa mashuhuda wazuri ambao tumekuwa tukishuhudia baadhi ya biashara nyingi zikifa hii ni kutokana na wahusika hao wamekuwa wakifanya biashara hizo kimazoea.
Lakini kumbuka acha mara moja kufanya biashara kimazoea kwani ukiendelea na tabia hiyo mafanikio yatakuwa yanajitenga nawe kila wakati.
Hivyo ili kuepuka kufanya biashara komazoea unahitaji aina hizi za elimu ambazo zitakusaidia kukua kwa kibiashara yako.
a) Elimu ya mawasiliano.
Hii ni elimu muhimu sana ambayo ni lazima mfanyabiashara yeyote yule anatakiwa kuwa nayo katika biashara yake.  Aina hii ya elimu huusisha dhima nzima ya jinsi ambavyo utawasilisha na wateja wako. 
Zipo biashara zimekuwa zikiendelea kufa kila kukicha hii ni kwa sababu wamiliki wa biashara hizo wamekuwa hawana aina hii ya elimu ya mawasiliano.

Pata elimu sahihi ya biashara, ukuze biashara yako.
Wengi wao wamekuwa wamesahau ya kwamba mteja huwa anavutiwa hasa pale ambapo unamjali hasa pale anapokuja katika biashara yako.  Ili uweze kukua kibiashara hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano mazuri kwa mteja wako.
Mawasiliano haya hutegemea hasa katika kauli zako. Kauli njema ni kuvutio kikubwa katika biashara.  Jifunze kuwa na lugha nzuri za kibiashara kama unataka kufanikiwa katika biashara yako.
Lakini vilevile kama hiyo haitoshi aina hii ya elimu ina ukaribu mbashara juu ya mmiliki wa biashara fulani kuweza kushirikiana na wafanyabishara wengine ambao wanaokuzunguka. 
Kufanya biashara bila kuwa na ukaribu na wafanyakazi wengine ni sawa na bure.  Hivyo nakusihi tu ya kwamba jitahidi kuwa na mawasiliano bora na wafanyabiashara wengine.
b) Elimu ya teknolojia.
Kwa kuwa sasa tupo ulimwengu wa utandawazi na vitu mbalimbali vimekuwa vikitengenezwa kila kukicha hivyo hakikisha unaendana na kasi hiyo.  Biashara yako ili ikuwe katika mstari wake,  unatakiwa kuifanya katika hali ya kisasa zaidi. 
Tumia vifaa mbalimbali vya kietroniki katika kujua mbinu za kuwa mbunifu kibiashara, na pia kujua namna ya kuongeza wateja hatimaye kuongeza mauzo.
Kwa mfano, unaweza kutumia simu yako kuwataarifu wateja wako kuhusu ujio wa bidhaa mpya.  Au unaweza kusoma mambo mbalimbali ambayo yanapatikana katika mitandao mbalimbali itakayokufanya uongeze wateja. Pia kumbuka maarifa hayana ukomo.
Itaendelea wiki ijayo siku kama ya leo.......
Ndimi Afisa Mipango : Benson Chonya,

No comments :

Post a Comment