Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, March 3, 2017

Mafanikio Yako Yamejificha Sana Hapa.

No comments :
Yapo matokeo ambayo katika maisha yako wewe huwezi kuyaona hapo hapo wala mwingine pia hawezi kuyaona kwako. Kwa mfano, unaposoma kitabu huwezi kuona matokea yake leo au kesho moja kwa moja, inachukua muda fulani.
Kwa hiyo unaona kama yapo matokeo ambayo huwezi kuyaona moja kwa moja, hapa ndipo unapotakiwa kuwa mwangalifu sana na maamuzi yote yote hasa katika vile unavyovifanya katika maisha yako.
Utake usitake, maamuzi yoyote yatakupa matunda au matokeo hata kama ni kidogo sana. Hapa sasa ndipo unapotakiwa ujue mafanikio kama mafanikio yanajengwa kwenye mstari mwembamba sana ambao wengi wanashindwa kuutambua.

Tofauti ya tajiri na maskini ndipo huanza kujitokeza, kwa mfano matajiri hujali sana kupata matokeo yasiyoonekana, tofauti na watu maskini ambao wao hutaka papo kwa papo, hutaka mambo yaonekane tu.
Kuwa makini sana na mambo unayoyafanya, kila jambo lifanye kwa faida, ili ukianza kuvuna matokeo usiyoyaona miaka kumi ijayo usije ukashikwa na mshangao, kwamba ‘alaa hivi kumbe nilikosea wapi.’
Ndio maana tunasema hivi hata yale maamuzi unayoyafanya leo, hayana uwezo wa kuathiri maisha yako kesho, kesho kutwa au mwakani, ila matokea ya maamuzi yako unaweza ukaanza kuyaona hata baada ya miaka mitatu, miaka mitano au hata zaidi ya hapo kabisa.
Kila wakati kuwa makini na maamuzi yako, kuwa na maamuzi ya busara. Kama utakuwa na maamuzi mabovu usishangae ukaja kukuta maisha yako tayari yameshaharibika na itakuwa ngumu sana kwako kuanza upya kurekebisha kwani itachukua muda pia.
Hakuna wa kukufanya ushindwe au kukuonea kwenye maisha yako. Kila kitu unacho wewe. Tambua kabisa yapo matokeo yasiyoonekana leo kwenye maisha yako, angalia matokeo hayo yasiweze kukupoteza.
Chunga matumizi yako ya pesa, angalia uhusiano wako na watu wengine, fanya kila unavyoweza kufanya kila kitu kiwe kwa ubora kwako hata kama huna matokeo yasiyoonekana. Matokeo hayo ipo siku yataonekna na yatakuwa nje.
Sasa usije ukawa miongoni mwa wale watakaolia kwa sababu ya kuvuna matokeo mabovu, ya mambo ambayo hawakutarajia yatakuja kuonekana. Fanya vitu vyenye maana, upate matokeo yanayoonekana mbeleni.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,


No comments :

Post a Comment