Mar 27, 2017
Namna Unavyoweza Kugeuza Makosa Yako Na Kuwa Mafanikio.
Makosa katika safari yoyote
ya mafanikio ni kitu ambacho
hakikwepeki. Bila shaka wewe na mimi tumeshawahi kukosea katika maeneo kadhaa
ya maisha yetu. Kukosea huko kulitufanya pengine tujute au kuumia kabisa na
kujiona kama vile hatufai.
Je, kitu cha kujiuliza hivi
ndivyo tulivyotakiwa kuyachukulia makosa haya na kujihukumu vya kutosha. Jibu
rahisi hapa ni hapana. Hatukuwa na sababu ya kujihukumu sana kutokana na makosa
yetu, zaidi ya kugeuza makosa hayo na kuwa ushindi.
Na ni kwa namna gani
tunaweza kugeuza makosa yetu kuwa ushindi?
1.
Jifunze kutokana na makosa hayo.
Ili
uweze kuwa mshindi na kugeuza makosa yako kuwa ushindi, ni lazima kujifunza
kutokana na makosa ambayo unayafanya. Kama hujifunzi, hakuna utachokuwa
unafanya, zaidi utaendelea kukosea na kubaki hapo. Wanaojifunza na kuchukua
hatua ndio wanaofanikiwa.
Kukosea
kwako hakuna shida sana, shida inakuja pale unaposhindwa kujifunza. Ni muhimu
kujifunza kutokana na makosa yako na kurekebisha pale ulipokosea. Kwa kadri
utakavozidi kujifunza utajikuta makosa yako yanageuka kuwa ngazi ya
kukufanikisha badala ya vizuizi.
USHINDI NI LAZIMA |
2. Chukua jukumu la kuwajibika.
Hautaweza
kwenda popote wala kupata mafanikio, ikiwa utakuwa ni mtu wa kulaumu wengine
kwamba ndio waliosababisha ukakosea. Mtu wa kwanza kuwajibika kwa makosa
uliyofanya ni wewe. Acha kulaumu wengine, utakuwa unapoteza wako bure. Wajibika
kwanza wewe.
Unapochukua
jukumu la kuwajibika elewa wewe ndiye kiongozi wa maisha yako, hivyo kama kuna
makosa yamefanyika kwa sehemu una mchngo wa kusababisha makosa hayo kujitokeza.
Badala ya kulaumu, tafuta nini kilichokufanya ukakosea, kirekebishe baada ya
hapo endelea na safari yko.
3. Jifunze kutokana na uzoefu.
Linaweza
likawa ni jambo linalokuuma sana, hasa pale unapokosea. Lakini nina uhakika
pamoja na maumivu hayo kuna kitu ambacho unaweza ukajifunza hapo. Kujifunza
huko, huo ndio uzoefu ninaotaka uuchukue hapo na kuugeuza kuwa ushindi pengine
yanapotokea makosa kama hayo kwa baadae.
Acha
kuishia kuumia na kulalamika na ukabaki hivyo, utakuwa hufanyi kitu. Utumie
uzoefu kukusaidia kufika kwenye kilele cha mafanikio. Mara nyingi kwenye
kipindi cha kukosea unaweza ukakiona ni cha mateso na maumivu. Lakini , kumbuka
siku zote uzoefu ni mwalimu mzuri w mafanikio yako.
4. Badili tabia zako.
Inawezekana
ukawa unashindwa na unaendelea kufanya makosa kwa sababu ya tabia ulizonazo.
Ili uweze kutoka hapo na kuepuka makosa huna namna nyingine zaidi ya wewe
kuweza kubadili tabia zako mara moja. Ukiweza kubadili tabia zako hizo zinazokurudisha
nyuma, basi yapo makosa ambayo unayarudia kuyafanya utayaepuka moja kwa moja na
kuwa mshindi.
Hivi ndivyo unavyoweza
kugeuza kushindwa kwako na kuwa ushindi wa mafanikio. Acha kuhuzunika na
kusononeka sana. Fanyia kazi mambo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwako sana.
Endelea
kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO na kumbuka tupo pamoja.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.