Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, March 9, 2017

Umuhimu Wa Kutumia Mbegu Na Zana Bora Kwa Mkulima.

No comments :
Ili kufanikiwa katika kilimo, kuna umuhimu mkubwa kwa mkulima kutumia mbegu na zana bora za kilimo ili kuleta tija kwa mkulima yeyote anayetaka kupata mafanikio hayo makubwa.
Kwa mfano mkulima inatakiwa kujiuliza kwa nini mbegu ya kawaida ya nyanya kama Mwanga,Tanya mbegu hizo zote kiasi cha 100g ambayo ndiyo ya kutosha ekari moja unaweza ukaipata kwa shilingi za kitanzania elfu 16-20 Lakini mbegu kama Faida F1 ambayo 60g inatosha ekari moja unaweza kupata kwa 150,000/=?
Utofauti wa hizo mbegu ni ustihimilivu katika magonjwa, kustahimili hali ya hewa, utofauti mkubwa wa mapato au mavuno shambani,yaani Faida F1 mavuno yake ni mara tatu zaidi ya mavuno ya mbegu ya kawaida, na unavuna kwa muda mrefu miezi 5-7 endapo utaendelea na matunzo.

Pia unakuta mkulima anayetaka mafanikio anaenda dukani anaulizia au anataka bomba/pampu/sprayer ya bei ndogo kabisa elfu 30-45 lakini akitumia kupulizia dawa hata ekari moja tuu utakuta anarudi dukani kutafuta spares, na wakati angeweza kupata sprayer yenye ubora kwa laki moja na bila kununua spares mara kwa mara.
Hivyo ili mkulima yeyote anayetaka mafanikio inatakiwa atumie mbegu na pembejeo za kilimo zilizo bora zaidi ili kufikia mafanikio makubwa zaidi. Kunielewa vizuri katika hili, leo ngoja nikuelezee kidogo kuhusu kilimo cha tikiti na uone umuhimu wa kutumia mbegu na zana bora za kisasa.
Katika kukuelezea kuhusu kilimo bora cha matikiti, naomba tutatumia mfano wa mbegu bora PATO F1.
MAHITAJI
Shamba ekari moja (4000 mita za mraba) liwe lako au la kukodi.
Ukipata shamba la tifutifu lililo changanyikana na mchanga itakuwa vema zaidi.   
Angalizo: Usilime matikiti kwenye udongo unaotuamisha maji yaani mfinyanzi kwani kama unavyoona udongo unavyo pasuka hivyo hata matikiti yakifikia hatu ya kukomaa yatapasuka pia.
Kiasi cha mbegu 250g yenye mbegu 5000 inatosha kupanda ekari moja.
HATUA ZA ULIMAJI.
Andaa shamba kwa kulima iwe kwa mkono au trekta lakini utifue kwenda chini angalau sentimita 15 kwenda chini.
Baada ya kulima liache shamba lipumzike baada ya hapo tumia kiua gugu non selective (Grypro ambayo itaangamiza nyasi zote ambazo zilikuwa zinaota, baada ya kupiga dawa liache kwa muda wa wiki moja hadi mbili ndiyo uende kupanda.
Kabla ya kuanza kupanda hakikisha unaanda mbolea ya kupandia yenye virutubisho vingi vya Phosphorus (P) kwa mfano DAP, Agrigrow starter NPK 14:28:18 kwa ajiri ya kupandia.
Panda mbegu kwa kuzingatia nafasi zifuatazo,mstari hadi mstari mita 2 na mche hadi mche sentimita 45.
Kwa siku 0-15 days (Planting) inatakiwa uwe na dawa ya wadudu Avirmec 1.8EC ambayo utatumia mls 7 kwa lita 20,na mbolea ya majani Agrigrow starter ,kwa sababu matikiti hupendwa sana na wadudu hiyo mbolea ya majani yenye virutubisho vingi vya Phosphorus ili kuufanya mmea uwe na mizizi imara na kuwezesha mmea kufyonza virutubisho vizuri kutoka kwenye udongo.
Siku 16-25(Vegetative /Trailing) tumia mbolea ya majani Agrigrow vegetative NPK 30:10:10. Hii mbolea itafanya miche ikue haraka haraka na kufanya uwe na matawi mengi au unaweza tumia Allwin top, na uwe na dawa ya wadudu Prosper 720EC (Profenofos 600g/L +Cypermethrin 120g/L),na mbolea za chini zenye virutubisho vya Nitrogen kwa wingi,dawa ya ukungu Agrilax 72WP.
Siku 25-40days(Flowering) hii ni hatua muhimu sana kwa mmea ambayo hata upigaji wa dawa hautakiwi upige wadudu wa muhimu wakiwa shambani,kwa mfano ukamkatisha nyuki akiwa anafanya kazi yake tunda litalotokea linakuwa halina umbo zuri(irregular shape)
Kwa kipindi hicho unatakiwa uwe na dawa za ya ukungu Agrilax 72WP,dawa ya wadudu Prosper 720EC na hakikisha unapiga dawa asubuhi sana au jioni sana,mbolea ya majani unaweza utumie Agrigrow flowering and fruiting ambayo itazuia kupukutika kwa maua,
Uwe na mbolea ya chini ambayo ina virutubisho vya Potassium kwa wingi
Siku 40-60-90days(fruiting) Uwe na dawa ya wadudu Avirmec 1.8EC (Abamectin),dawa ya ukungu Agrilax,mbolea ya majani Agrigrow flowering and fruiting au Allwin top ambayo itaboresha tunda na ubora wake.
Pia wakati huo uwe na mbolea ya chini yenye virutibisho vingi vya Potassium.
MAVUNO.
Baada ya hapo tuangalie idadi ya miche abayo utatarajia kuwa nayo na idadi ya matunda ambayo utatakiwa uyavune kwa ekari moja.
Idadi ya miche inapatikana kwa formula/Kanuni maalumu ambayo ni;-
Plant population (PP) =Area(1acre,4000m square) divided by Spacing times number of seeds per hole
      Au
Miche =Eneo(ekari moja) ÷nafasi ya upandaji zidisha na mbegu utazokuwa unaweka kwa kila shimo.
Area/Eneo ni 1acre/ekari moja ambayo ina ukubwa wa 4000mita za mraba.
Nafasi kati ya mstari hadi mstari ni mita 2(2m) ,mche hadi mche ni sentimita 45(45cm) or 0.45m,na inatakiwa upande mbegu moja moja tu.
Kwa hiyo
    PP=Area/Spacing ×number of seeds per hole
 PP=((4000/(2×0.45))×1
 PP=4,444plants/acre
 PP=4,444plants.
Kwa hiyo kutakuwa na miche 4,444 kwa ekari moja.
Na kwa kawaida tikiti la hybrid (PATO F1) huzaa matunda kuanzia 5-7 na muda mwingine yanaweza kufikia hata 10 ,ila tunamshauri mkulima apunguze matunda na kuyaacha matunda matatu tuu kwa kila mche.
Tunamshauri mkulima kupunguza matunda ili kupata matunda matatu tu, kwa mche mmoja ambayo yatakuwa na ubora,na kuyauza kwa bei nzuri.
Kwa hyo basi kama mche mmoja utakuwa na matunda matatu yaliyo bora. Je utakuwa na matunda mangapi kwa ekari,hebu tuangalie hesabu hii chini;-
1plant= 3ftuits
4,444plants= x?
Therefore=4,444×3
       =13,332fruits/acre
Kwa hyo utagundua kuwa unatakiwa uwe na matunda 13,332 kwa ekari moja.
Kama sehemu uliyopo wananunua tikiti hata kwa bei ya chini sh 500,utakuwa na jumla ya pesa 500×13,332=sh 6,666,000/=
Kama wananua kwa sh 1000 basi utakuwa na sh 1000×13,332=sh 13,332,000/=
Kama wananua kwa sh 1500 utakuwa na jumla ya pesa 1500×13,332=sh 19,998,000/=
Kama utaweza kupata soko zuri zaidi kwa bei ya sh 2000 basi utakuwa na jumla ya sh 2000×13,332=26,664,000/=
Na kwa wale wanaouza kwa kilo kwa mfano bhakresa hununua tikiti kwa kilo,hili tikiti la PATO F 1 baada ya kulivuna linakuwa na lilo 8-15.
Makala hii imeandikwa na Boniface L Pwele mtaalamu wa kilimo. Kwa ushauri wa kilimo cha kisasa, ununuzi na utambuzi wa mbegu bora, wasiliana nae kwa blugahno95@gmail.com au mpigie kwa+255 762 56 76 28.

No comments :

Post a Comment