Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, March 17, 2017

Tumia Mbegu Bora Ukuze Kipato Chako.

No comments :
Leo tunaendelea na umuhimu wa kutumia mbegu bora kwa mkulima yoyote anayetaka mafanikio ni lazima atumie mbegu bora ili kuyaendea mafanikio. Mbegu bora ndio msingi wa mafanikio kwa mkulima.
Naomba bila kupoteza muda tuangalie utofauti uliopo kati ya mbegu ya kawaida (Open pollinated varieties OPV) na mbegu chotora (Yaani Hybrids seeds) na ni nini faida yake kwa mkulima akishajua tofauti hizo.
Kwanza katika uotaji,mbegu ya kawaida ina husua sua katika uotaji yaani uotaji wake ni shida lakini mbegu chotora zina uhakika mkubwa sana wa kuota na mkulimahupotezi pesa yako ukinunua.
Ukichunguza kwa kina utagundua ndiyo maana mbegu nyingi chotara ukiuziwa uliza kabisa kuna mbegu ngapi humu ingawa zingine zimeandikwa idadi ya mbegu. Hiyo yote inaonyesha uhakika wa mbegu hizo.


Ustahimilivu wa magonjwa,Mbegu chotara huwa zina vumilia magonjwa yaani hazishambuliwi ovyo na magonjwa ukitofautisha na mbegu za kawaida hushambuliwa kirahisi na magonjwa.
Ubora wa bidhaa, mbegu chotara huwa na ubora zaidi baada ya kuvuna ukitofautisha na mbegu ya kawaida. Ndio maana wakulima wengi wenye mafanikio, hutumia sana mbegu hizi.
Mavuno ya mbegu chotara huwa zina mavuno mengi ukitofautisha na za kawaida. Mavuno haya mara nyingi huwa ni makubwa na kumfanya mkulima kunufaika na kipato atakachokipata.
Pia mbegu chotara hutoa mavuno mengi na yaliyo bora (High yield and quality) lakini za kawaida mavuno kidogo na siyo bora kama ya chotara(Low yield and not quality)
Kwa mfano mbegu ya nyanya FAIDA F1 3169 na FAIDA F1 3104 huweza kuvunwa zaidi ya miezi sita na huzaa matunda mengi sana. 
Hivyo hata katika soko huwezi pambana na mtu aliyelima mbegu za kawaida na aliye lima mbegu chotara, kwa mfano mtu atakaye lima nyanya mfano tanya hawezi fanana na mtu aliye lima FAIDA F1 NTH 3104 au FAIDA F1 NTH 3169.
Pia hata Yule aliye lima FAIDA F1 atauza bei ya juu (mara mbili au mara tatu zaidi) kuliko aliye lima nyanya ya kawaida, kwa kuwa zina ubora ulio tofauti. Kwa hilo hiyo mkulima hawezi kupata hasara kirahisi.
Naomba sana utambue hivi ili uweze kuingia katika kilimo na ukapata matokeo chanya, hutakiwi kukurupuka. Kaa chini, utulie, fanya uchunguzi wale wanaofanikiwa kwenye kilimo wanafanya nini cha ziada.
Kilimo cha manufaa hakiendeshwi kwa mihemuko au kwa whats app. Unataka kulima na umelenga kupata matokeo mazuri na hujui wapi pa kuanzia waone wataalamu wa kilimo.
Kazi kwako kwa wewe mkulima unaye taka mafanikio, tumia mbegu bora (Hybrid seeds) zikuletee mafanikio. Tukutane wiki ijayo kwa makala nyingine nzuri ya kilimo.
Wako mtaalamu wa kilimo,
Boniface L Pwele.                       
Kwa msaada zaidi wa kuendesha kilimo chenye  mafanikio, usisite kuwasiliana nasi. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0762567628 au tuma ujumbe kwa barua pepe blugahno95@gmail.com


No comments :

Post a Comment