Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, March 29, 2017

Hawa Ndio Wanawake Waliofanikiwa Sana Kwenye Ujasiriamali.

No comments :
Siku zote tunasema na tutaendelea kusema  kwamba mafanikio hayana rangi, kabila, umri wala jinsia, ukiamua kufanikiwa kwa vyovyote vile ulivyo hata uwe katika kona gani ya dunia utafanikiwa tu, kwa sababu umeamua iwe hivyo kwako na itakuwa.
Nasema hivyo kwa sababu, mara nyingi watu wengi linapokuja suala la mafanikio huwa kuna bagua bagua nyingi sana kwa upande wao. Kwa mfano, mtu anakwambia kabisa huwezi kufanikiwa kwa sababu wewe umri wako ni mdogo au huwezi kufanikiwa sana kwa sababu wewe ni mwanamke.
Ukiangalia ukweli wa mambo ulivyo kwenye mafanikio hauko hivyo, kwa vyovyote vile ulivyo unaweza ukafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa bila kujali unaishi nchi gani au bila kujali wewe ni mtu wa jinsia gani yaani mwanaume au mwanamke.
Kutilia mkazo katika hilo na ili unielewe vizuri ninachosema hapa, leo kupitia makala haya tuangalie baadhi ya wanawake ambao wamepata mafanikio makubwa sana duniani kupitia ujasiriamali, ingawa kuna wakati pengine walibezwa na kukejeliwa sana kwamba hawawezi kufika popote.
1. Oprah Winfrey
Pamoja na kwamba Oprah kwa sasa ameshaacha mambo ya utangazaji kwenye televisheni lakini ni moja ya wanawake ambao wamefanikiwa sana na kuwa na pesa nyingi kutokana na kujituma na kuwekeza kadri alivyoweza hadi kufikia mafanikio aliyonayo sasa.
Yeye kama yeye kupitia kituo chake cha Oprah Winfrey leadership academyamefanikiwa kuwasaidia watoto wengi wa kike, pia ni jambo ambalo limekuwa llikimuungizia pesa za kutosha. Ameidhirihishia dunia kwamba mafanikio hayana jinsia ni kujituma tu.

2. Folorunsho Alakija
Alakija ni moja pia ya wanawake wenye pesa na tajiri sana nchini Nigeria. Biashara zake zilizompa utajiri ni biashara ya mapambo na mafuta. Kwa sasa Alikija anakadiriwa kufikia utajiri wa dola za kimarekani billion 1. 6.
Mpaka hapo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo naye amejitahidi kuweka juhudi nyingi za kufikia mafanikio yake aliyonayo katika kile anachokifanya. Hiyo yote inaonyesha juhudi ikiwekwa popote hakuna kinachoshindikana.

3. Wang Laichun
Laichun pia inasemekana ni moja ya mabillionea wa kichina ambapo utajiri wake alionao ambao kwa sasa unafikia dola za kimarekai bilini 1.67, umetokana na juhudi zake binafsi na sio kurithi.
Biashara iliyompaisha hadi kufika huko aliko sasa ni biashara ya vifaa vya umeme ambavyo anavisambaza na amekuwa mojawapo ya wanawake matajiri sana duniani.

4. Debbie Fields
Pia katika wanawake wajasiriamali na wenye pesa huwezi kumsahau mwanadada huyu Debbie fields katika ulimwengu wa mafanikio. Ni moja ya wanawake kweli waliofanikiwa haswaa.
Utajiri wake hasa ni wa nini? Huu ni mwandada anayejihusisha na kutengeneza vyakula vya aina tofauti tofauti vyenye mfumo kama wa keki. Ambapo kwa sasa anasambaza vyakula vyake zaidi ya nchi kumi duniani. 
Mafanikio katika maisha yako yanawezekana. Huna haja ya kuwa na sababu kwamba mimi sina hiki au kile au mimi kwa sababu ni jinsia hii siwezi kufanikiwa, weka juhudi, matokeo utayaona.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspt.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment