Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, March 1, 2017

Ukifahamu Vyema Mambo Haya, Utajiri Ni Wako.

No comments :
Zipo sheria au mambo ambayo watu wengi wenye mafanikio wanayafahamu na kuyatumia kama ngazi ya kuufikia utajiri wao. Haijalishi mambo hayo au sheria hizo umezitumia kwa kukusudia au kwa bahati mbaya ila ukizitumia tu unafanikiwa.
Leo kupitia makala haya nataka nikushirikishe mambo muhimu ambayo ni muhimu sana kwako, lakini ambayo ukiyatumia yatakusaidia moja kwa moja kuweza kufikia mafanikio makubwa hadi utajiri wako.
Twende pamoja kujifunza kupitia mambo hayo;-.
1. Fanya mambo yako kwa utofauti.
Hakuna uchawi katika mafanikio mkubwa kama huu, kama unafanya vitu vyako kwa utofauti, ni lazima utapata mafanikio makubwa. Watu wote wanaofanya mambo kwa utofauti wanafanikiwa bila pingamizi lolote.
Haijalishi una pesa au huna. Haijalishi una mtaji au huna. Haijalishi una kipaji au huna, lakini wewe fanya mambo yako kwa utofauti utapata mafanikio makubwa sana ambayo hata hukutegemea.

2. Waza chanya wakati wote.
Kufikiri na kutenda kwa utofauti mara nyingi kunatokana na jinsi unavyowaza. Je, unawaza nini kichwani mwako? Kichwa chako kina kitu gani hiyo ndiyo itakayokufanya ufanikiwe.
Waza umefanikiwa hata kama ndani yako huoni kitu. Waza unaona una afya tele hata wakati ambao unaona wazi kabisa bado hujapona. Mawazo yako yana nguvu kubwa sana ya kukufanya ufanikiwe. Yatumie vizuri yakusaidie kufanikiwa.
3. Jenga picha kamili ya kile unachokitaka.
Mafanikio makubwa sio uchawi ni sayansi. Unataka kufanikiwa itumie sayansi hii kwa kujiwekea picha sahihi ya kile unachokitaka kichwani mwako. Kijue vizuri kile unachokitaka bila kubababisha hata kidogo.
Kijue kile unachokitaka kama vile unavyojua gari lako, nyumba yako au sehemu yoyote ile unayoifahamu. Kama kitu hicho unakijua kwa namna hiyo ni rahisi kuweza kukivuta na kuwa upande wako.
4. Kuwa mtu shukrani.
Kwa watu wengi hiki kinaweza kuonekana ni kitu cha kawaida kabisa lakini shukrani yoyote ina nguvu kubwa sana na muunganiko na mafanikio yako. Unapokuwa ni mtu wa shukrani unakuwa unavuta mafanikio mengine zaidi bila ya wewe kujielewa.
Kama unaishi maisha ya kutokuwa na shukrani unakuwa unavunja uhusiano moja kwa moja na Mungu wa mafanikio. Hebu jifunze kuwa na shukrani, hata biblia imeandika sana kuhusu hili jambo la kuwa na shukrani.
5. Acha kuongelea umaskini kabisa.
Umaskini hauwezi kutoka kwako eti kwa sababu unajifunza juu ya umaskini na sababu zake. Hauwezi kupata kitu kwa kujifunza kinyume chake. Unataka kuwa tajiri jifunze juu ya utajiri na yale yote wanayofanya matajiri na sio ujifunze umaskini.
Hivyo kwa vyovyote vile acha kuwaza au kuongelea umaskini. Wewe na umaskini sio watu marafiki. Jifunze juu ya utajiri na mambo yanayopelekea hadi mtu mwingine akawa tajiri kwenye maisha.
6. Chukua hatua mara moja.
Weka akili na mawazo yako yote kwenye kuchukua hatua moja kwa moja. Acha biashara ya kuahirisha na kusema nitafanya hiki kesho au kesho kutwa hebu fanya sasa hilo unalotaka kulifanya leo.
Kama kuna sehemu ulikuwa umekosea jana hiyo ilikuwa ni jana. Lakini lilokubwa kwako ni kuchukua hatua mara moja za utendaji bila kuangalia mazingira uliyopo. Kama unasubiri mazingira yakae sawa, yatakaa sawa wakati huku ukiendelea kutenda.
Hakuna atakayeshindwa kufikia mafanikio ikiwa unatumia mambo hayo vizuri ya mafanikio kwa ufasaha. CHUKUA HATUA.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
dirayamafanikio.blogspot.comNo comments :

Post a Comment