Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, March 14, 2017

Ongeza Maarifa Na Badili Maisha Yako,..Kupitia Hamasa Hizi Muhimu Kwako.

No comments :
Kati ya nguzo mojawapo kubwa ya mafanikio ni hamasa. Huwezi kufanikiwa bila kuwa na hamasa hata kama una rasilimali nyingi vipi za kukusaidia kufanikiwa, itafika mahali utashindwa.
Kwa kuwa hamasa ni muhimu katika mafanikio yoyote yale, hebu leo hii kupitia makala haya tujifunze pamoja baadhi ya hamasa ambazo zitakusaidia kuweza kupiga hatua ya kimafanikio.
Hamasa ya 1.
Katika dunia ya sasa, taarifa nyingi za ni nini ufanye au kipi usifanye ili uweze kufanikiwa, tayari zipo. Kazi kubwa uliyonayo, ni kutumia taarifa hizo ili ziweze kukusaidia kufanikiwa.
Watu wengi wanashindwa kwenye maisha si kwa sababu hawana taarifa sahihi za mafanikio, bali ni kwa sababu hata zile taarifa kidogo walizonazo hawazitumii kuweza kuwasaidia kufanikiwa.
Acha kulalamika kila wakati kwamba eti huzioni fursa, kama ni fursa, zipo nyingi na za kutosha. Tatizo kubwa ulilonalo ni kule kwa wewe kushindwa kuchukua hatua ya kuzitumia fursa hizo kwa uhakika ili zikupatie mafanikio.
Ongeza hamasa yako kila siku.
Hamasa  ya 2.
Kuchukua hatua na kuweka juhudi hiyo peke yake haitoshi ili kufikia mafanikio makubwa. Unatakiwa kuongeza kitu cha ziada ambacho ni MTAZAMO SAHIHI. Hiki ndicho kitu unachotakiwa kukiongeza wakati unachukua hatua na kuweka juhudi.
Unapokuwa na mtazamo sahihi, huku ukichukua hatua na kuweka juhudi zote kwa kile unachokifanya, lazima utafanikiwa. Watu wote wenye mafanikio wana mitazamo mingi sahihi inayowapa nguvu ya kufanya tena na tena hadi kufanikiwa.
Hamasa  ya 3.
Maisha ya mafanikio yanaundwa na vitu vidogo vidogo sana. Zile hatua ndogo kabisa ambazo unaziona haziwezi kukusaidia kufanikiwa, hizo ndizo zinaweza kukupa mafanikio kama utafanya kwa muda mrefu.
Hebu kama kuna kitu unataka kukifanya, anza kukifanya bila kujiuliza uliza. Acha kabisa kuahirisha mambo yako, utakuja kujuta sana baadae utakuwa umepoteza pesa nyingi na mafanikio kwa ujumla kwa sababu ya kuahirisha.
Ipo gharama kubwa sana ya kusubiri subiri na kuahirisha mambo kuliko unavyofikiri. Utapoteza mambo mengi sana ambayo moyo wako utakuuma sana na kujiuliza kwa nini ulisubiri na hujufanya mapema. Fanya na acha tena kusubiria kitu au kuahirisha.
Hamasa  ya 4.
Tofauti kubwa kati ya watu wenye mafanikio na wasio na mafanikio, haipo kwenye kurithi, kipaji au uwezo mkubwa sana. Tofauti kubwa inajitokeza kwenye kufanya yale mambo ambayo yanaonekana ni rahisi.
Hili ndio kosa ambalo watu wenye mafanikio hawafanyi. Yale mambo ambayo yanaonekana ni madogo na ya kudharaulika kabisa wao wanayafanya bila shida yoyote na ndio yanayowapa mafanikio makubwa.
Hata ukiangalia watu wenye mafanikio na watu wasio na mafanikio wanafanya mambo yale yale ambayo yanafanana kwa siku kwa mfano kula, kusoma kitabu cha aina moja na kuhudhuria semina.
Tofauti inaanza kujitokeza hasa pale kwenye umakini wa kutumia hasa mambo yale wanayojifunza karibu kila siku. Umakini hapa sasa, ndio unawatenga waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa.
Hamasa  ya 5.
Kuna vitu vitatu ambavyo unatakiwa uwe navyo ili uweze kupata kile unachokihitaji katika maisha yako. Vitu hivi ni lengo maalumu kwa kile unachokitaka, maarifa ya hicho unachokitaka na hamasa ya kupata kitu hicho. Hayo ni mambo ya lazima sana ili uweze kupata kitu unachokitaka kwene maisha yako.
Najua kuna kitu muhimu umejifunza hapa cha kuweza kukusadia kubadili maisha yako. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspt.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,


No comments :

Post a Comment