Sep 9, 2015
Hivi Ndivyo Vizuizi Vikubwa Vinavyokufanya Ushindwe Kufanikiwa.
Wengi
wetu siku zote huwa ni watu wa kutafuta mafanikio. Jambo hili tunakuwa
tunaliona hasa kutokana na shughuli zetu
tunazozifanya kila siku ambazo zinakuwa zinalenga mafanikio hayo tunayoyataka.
Hakuna mtu ambaye anakuwa hatamani mafanikio, kila mtu anakuwa ana hamasa ya
kutaka mafanikio katika maisha yake tena kwa nguvu zote bila kuchoka.
Lakini
pamoja na wengi wetu kuwa na nia hii ya kutaka mafanikio hayo, huwa siyo rahisi
kuyafikia. Hili mara nyingi linakuwa linatokea hivyo kutokana na safari ya
mafanikio kuwa na changamoto zake ama vizuizi ambavyo ni lazima uvivuke ili
kufanikiwa. Wengi wanapokutana na vizuizi hivi hujikuta wamekwama na unakuwa
ndiyo mwisho wao hapo.
Inapotokea
umekutana na vizuizi hivi visije vikakufanya ukabaki na huzuni na kujiona hufai
tena ama una mkosi. Kitu kikubwa cha kufanya jifunze, kisha chukua jukumu la
kusonga mbele. Tambua, ni lazima kuvielewa vizuizi hivi ili kujua namna ya
kukabiliana navyo na kwenda upande wa pili wa mafanikio, la sivyo utakwama kila
siku.
Je,
ni vizuizi vipi hivi?
1. Kukosa mipango na malengo.
Watu
wengi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao makubwa kutokana na kukosa
mipango na malengo iliyothabiti. Hiki ni kitu ambacho kimekuwa kikiwakwamisha
watu wengi sana katika safari yao ya mafanikio. Ili kuweza kufanikiwa ni lazima
kuwa na mipango na malengo imara. Kuwa na mipango na malengo ndiyo dira yako
kubwa ya kukufanikisha.
Huwezi
kufanikiwa kwa lolote kama utakuwa huna vipaumbele unavyotakiwa kuvitekeleza.
Siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye vipaumbele unavyojiwekea katika maisha yako kila siku.
Kizuizi kimojawapo kinachopolekea ndoto za wengi kutokutimia ni kushindwa
kujiwekea vipaumbele hivi, ambavyo ni muhimu kwa mafanikio yao.
3. Kuahirisha mipango.
Hili
ni tatizo kubwa sana linalowakabili wengi wetu bila kujijua. Wapo watu ambao
mara nyingi wanatabia ya kusema nitafanya hiki kesho, na inapofika kesho hiyo hawafanyi
tena. Watu hawa hujikuta ni watu wenye kuahirisha mambo mengi sana karibu kwenye kila jambo
kwenye maisha yao. Kwa tabia hii ya kuahirisha mipango yao wamekuwa wakijiwekea
kizuizi kikubwa kwenye mafanikio yao bila kujua na malengo yao kutotimia kabisa.
Ili kufanikiwa ni muhimu kuachana na tabia ya kuahirisha mipango.
4. Kukosa nguvu ya uzingativu.
Pia
hiki ni chanzo kikubwa cha malengo mengi ya watu kutokuweza kutimia katika
maisha yako. Kwa kawaida ili uweze kufanikiwa unahitajika kuweka nguvu zako
nyingi za uzingativu katika eneo moja mpaka upate kile unachokihitaji au
matokeo unayoyataka. Sasa tatizo la wengi hawafanyi hivi na matokeo yake
kusababisha malengo yao kutotimia siku zote.
5. Kuacha kushikiria malengo mpaka mwisho.
Wengi
linapotokea tatizo huwa ni rahisi sana kwao kushindwa kung’ang’ania malengo yao mpaka
kupata kile wanachokihitaji. Wengi hujikuta ni watu wa kuishia kati na kukata
tamaa. Kwa mtindo huu wa maisha suala la kufanikiwa linakuwa gumu sana kuwezekana. Hii ni kwa
sababu mafanikio yanataka kwa kiasi kikubwa uwe na uwezo wa kung’ang’ania mpaka
ufanikiwe. Kinyume cha hapo sahau mafanikio hayo.
6. Kutokujitoa.
Kujitoa
ni moja kati nguzo kubwa sana ya mafanikio katika maisha ya mwanadamu. Wengi wetu
huwa ni watu wa kutaka mafanikio bila kujitoa kikamilifu ili kufikia mafanikio
hayo. Kama unaishi maisha haya ya kutokujitoa suala la kuwa na mafanikio
makubwa katika maisha yako litakuwa kigumu kidogo kutokea.
7. Kukosa mafunzo.
Kutokana
na wengi kukosa mafunzo muhimu ya kuwasaidia kufanikiwa hujikuta ni watu wa
kukwama kila siku katika maisha yao. Ili uweze kufanikiwa unahitajika kujifunza
kila siku. Kujifunza huko unatakiwa kujifunza kupitia vitabu, semina na warsha
mbalimbali ambazo zinaweza zikawa ni muhimu kwako ili kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.
8. Kukataa mabadiliko.
Haiwezekani
hata kidogo ukaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ikiwa wewe mwenyewe hutaki
kutambua mabadiliko muhimu yanayoendelea katika maisha ya kila siku. Maisha
yanabadilika na yataendelea kubadilika siku zote. Hivyo ni lazima kwako kuweza kubadilika
ili kuendana na kasi ya maisha, vinginevyo utaachwa nyuma sana kiasi kwamba
utabaki unashangaa.
9. Kukata tamaa.
Hiki
pia ni kizuizi kikubwa sana ambacho wengi kinawakwamisha katika harakati zao
za kuelekea kwenye mafanikio. Wengi wetu huwa ni watu wa kukata tamaa
tunapokutana na magumu. Hali hiyo inapojitokeza suala la kusonga mbele na
kufanikiwa linakuwa siyo rahisi hata kidogo kuweza kutokea katika maisha yako.
10. Hofu ya kushindwa.
Wapo
watu ambao mara nyingi huwa na nia ya kufanikiwa, lakini kinachowazuia kufanya
hivyo ni kutokana na ile hofu yao kubwa waliyonayo ndani mwao ya kuogopa
kushindwa. Hofu hii mara nyingi inakuwa inajitokeza pale unapotaka kufanya
jambo jipya. Kwa kuwa na hofu hii tu, wengi hujikuta wamekwama kufikia malengo
yao makubwa.
Kushindwa
kwa mtu katika maisha yake mara nyingi kunasababishwa na vizuizi vingi sana ikiwemo hivyo ambavyo tumejifunza.
Bila kuwa makini na kuchukua hatua imara za kukabiliana na vizuizi hivyo, itakuwa ni kitu kisichowezekana kuyafikia
mafanikio unayoyahitaji siku zote. Chukua hatua na tafakari.
Nakutakia
ushindi katika mabadiliko juu ya maisha yako na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.