google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 15, 2015

Sababu Tano Kwanini Ni Muhimu Sana Kwako Kutimiza Malengo Uliyojiwekea.

No comments :
Kati ya kitu ambacho unatakiwa kukifatilia kwa ukaribu sana  katika maisha yako na kukifanikisha  ni malengo yako uliyojiwekea. Unapokuwa umejiwekea malengo yanakuwa yanakupa dira, nguvu na mwelekeo wa kukusaidia kusonga mbele na hatimaye kuwa na mafanikio ya hali ya juu.
Hakuna mafanikio yanayoweza kutokea kama hujiwekei malengo. Mafanikio yote yawe makubwa au madogo yanaanza na kujiwekea malengo. Bila kujiwekea malengo na kuyatimiza maisha yako inakuwa ni kama kazi bure.  Kitu cha kujiuliza hapa, ni kwanini ni muhimu na lazima kwako kuweza kutimiza malengo yako?
Zifuatazo Ni Sababu Tano Kwanini Ni Muhimu Sana Kwako Kutimiza Malengo Uliyojiwekea.
1. …Yanakupa ujasiri wa kutenda zaidi.
Kile kitendo cha kujiwekea malengo na kufanikisha kinakuwa kinakupa ujasiri mkubwa wa kutenda zaidi. Hebu hapo ulipo, jaribu kufikiri jambo ambalo umewahi kulifanya na kulifanikisha. Kila unapolikumbuka linakuwa linakupa nguvu na ishara ya kuwa hata mengine unaweza ukayafanya tena kwa mafanikio makubwa. Hii ndiyo siri na faida kubwa ya kutimiza malengo yako.

2. …Yanakuwa kipimo cha mafanikio yako.
Kutimiza malengo uliyojiwekea ni kipimo tosha kabisa cha kule unakotaka kufika kimafanikio. Kwa kuwa ulijiwekea malengo na umeyafanikisha inakuwa rahisi kwako kugundua ni maeneo yapi ambayo unatakiwa kuyasimamia vizuri ili kujiandaa kwa ajili ya safari nyingine mpya ya malengo. Hivyo, kufanikisha malengo ni kama pima joto ya mafanikio yako kuonyesha wapi ulipo na unakwenda wapi sasa.
3. …Yanakuwa msaada kwa wengine.
Ni jambo ambalo unalotakiwa ulijue ya kuwa tunaweka malengo si kwa ajili yetu tu, bali pia na kwa wengine wanatuzunguka ili tuwe msaada kwao. Kufanikisha malengo yako na kunufaika nayo wewe mwenyewe na kusahau jamii inayokuzunguka kwa karibu, hiyo inakuwa sawa na kazi bure. Kwahiyo, ni lazima kutimiza malengo ili kuwa msaada kwa wengine pale inapohitajika.
4. …Yanakupa changamoto.
Kile kitendo cha kutimiza malengo uliyojiwekea ni lazima kuna changamoto ambazo ulipitia. Kupitia changamoto hizo, naamini hazikukuacha bure kuna kitu ulijifunza cha kukuboresha zaidi. Kwa hiyo kuna ukomavu au uzoefu ambao unakuwa umepitia hapo, lakini ambao ukiuangalia umetokana na malengo yako uliyojiwekea ingawa umeyafanikisha.
5. …Yanakupa furaha.
Hakuna mtu ambaye anatimiza malengo yako, halafu ndani yake akakosa furaha. Ile hatua ya kuwa na malengo yako, halafu ukayatimiza ni furaha kubwa sana. Kwa hiyo utaona kuwa kwa kadri unavyoendelea kutimiza lengo hili na lile katika maisha yako unakuwa unajijengea furaha kubwa na ya kudumu maishani mwako inaendana na ujasiri mkubwa.
Kufanikisha malengo yako uliyojiwekea ni jambo linalokupa manufaa mengi kwako siku hadi siku ikiwa ni pamoja na kukujengea uzoefu ambao utakuwa unatembea nao siku zote za maisha yako.
Kwa leo naomba tuishie hapa rafiki, tukutane tena katika siku nyingine kwa ajili ya kujifunza na kuboresha maisha yetu kwa pamoja.
Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
 Ni wako rafiki katika mafanikio,
 Imani Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035 kwa ushauri na msaada wa haraka.  


 




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.