google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 4, 2015

Jifunze Jinsi Ambavyo Unaweza Kuwa Mhamasishaji Mkubwa.

No comments :
Zipo ndoto nyingi sana ambazo sisi binadamu tunakuwa nazo katika maisha ya kila siku. Wapo ambao wanapenda kuwa madaktari, marubani, walimu na hata wapo wanaopenda kuwa wahamasishaji wa kimataifa ingawa ni wachache lakini wapo.
Unapoamua kuwa mhamasishaji maana yake katika maisha yako umeamua kuwatia moyo wengine kupitia maandishi yako au kile unachotaka kukizungumza moja kwa moja katika jamii yako. Unakuwa hauna tofauti sana na wahubiri wa injili tofauti yake wewe unakuwa unahubri injili ya mafanikio.
Tunaona katika Dunia ya leo wapo wahamasishaji wakubwa kama vile akina Brian Triacy, Donald Trump, Robert Kiyosaki, Dale Carnegie, Bo Sanchez na wengineo wengi ambao wameamua kuisadia Dunia kwa sehemu kubwa kutokana na kile wanachosema kupitia maandishi yao au vinywa vyao.
Wapo watu wengi sana ambao hawakuwa na matumaini na mafanikio, lakini wamepata mafanikio na kufanikiwa kusonga mbele kimaisha baada ya kuwasikiliza au kuwasoma watu hao. Tena wakati mwingine wanafanikiwa hata watu hao ambao ni wahamasishaji wanakuwa hawana habari.
Inawezekana na wewe ukawa moja kati ya watu wenye ndoto kama hizi kubwa katika maisha yako na kuwa mhamasishaji mkubwa wa mambo mbalimbali katika jamii zetu ikiwa pamoja na mafanikio.
Ni jambo nzuri kwa sababu unakuwa unatoa mchango moja kwa moja kwa jamii kupitia ujuzi ulionao, hiyo inakuwa ni sawa na kutoa sadaka ambayo baadae itakurudia kwa namna tofauti. Na ukumbuke pia unapowasamasisha wengine, inakuwa unajipa nguvu ya wewe ya kuweza kufanikiwa zaidi.
Lakini kama ilivyo kwa mambo mengine huwezi kuwa mhamasishaji mkubwa mpaka ujifunze kujenga misingi imara na thabiti kunzia leo. Hicho si kitu cha kukurupuka kama utafanya hivyo ni wazi utadondoka ikiwa hutajiandaa kusimama vizuri.
Kujiandaa huku inaweza ikawa ni kujisomea vitabu ama kuangali yale wanayofanya. Ukumbuke kuwa utakuwa unaongea au kuwaandikia  watu wengi pengine zaidi ya elfu mbili  hivi, kwa hiyo maandalizi yanahitajika tena kwa lazima.
Ni mambo gani ambayo unatakiwa kuyazingatia kwa sasa ili uweze kuwa mhamasishaji mkubwa na bora zaidi?
1. Anzia pale ulipo.
Anza kuzungumza na watu ulionao katika mazingira uliyopo. Kama kuna kitu ambacho unapenda kuwapa cha kuwahamasisha na kikawafanya wabadili maisha yao wape kitu hicho bila ya kuogopa wala kusita. Kama umeamua kuandika andika kwa ajili yao au kama umeamua kuzungumza zungumza pia kwa ajili yao mpaka maisha yao yabadilike. Hivi ndivyo unavyoweza kuanza kwa hatua za mwanzoni kuwa mhamasishji mkubwa na mwenye mafanikio.

2. Chukua somo ambalo watu wanapenda kulisikia.
Ni vyema katika mada zako ambazo unataka kuzitoa, hakikisha unalenga somo ambalo watu wanapenda kulisikia. Kama ni mafanikio, hakikisha unatoa mada ambayo inagusa jamii yako na kutatua matatizo makubwa na kuwaweka watu hao huru. Kwa kufanya hivyo utawavuta wengi ambao watatamani tena kusikia kwako mambo mengi ya mafanikio. Na hivyo ndivyo ambavyo utakuwa unajenga misuri taratibu ya kuwa mhamasishaji mkubwa.
3. Jifunze kutoa mada kwa wengine bila gharama.
Kama umeamua kutoa mada kwa njia ya semina mwanzoni fanya semina hizo bila gharama yoyote ile au weka gharama za kawaida zisiwe kubwa sana. Hii itakusaidia kukupa uzoefu na itakujengea nguvu kubwa ya kujiamini hali itakayosababisha au kukupelekea wewe kuwa mhamasishaji mkubwa.
Kwa kufanyia kazi mambo hayo matatu yanauwezo mkubwa kabisa wa kukufanya ukawa mhamasishji mkubwa na mwenye mafanikio makubwa na ambaye unaingiza kipato kikubwa.
Nakutakia  ushindi katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea  DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuboresha maisha yako kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.