Nov 1, 2016
Njia Zinazotumiwa Na Wengi Kufikia Mafanikio Makubwa.
Mara nyingi linapokuja
swala la kufikia mafanikio makubwa, nguvu ya uzingativu, uwezo wa kufanya kazi
kwa bidii na ung’ang’anizi, ni mambo yanayotajwa sana kwamba yana mchango
mkubwa wa kusaidia kufikia kwenye mafanikio makubwa.
Hata hivyo,pamoja na
mambo hayo kuwa yana umuhimu na msingi mkubwa katika kufikia mafanikio makubwa,
pia zipo njia nyingine ambazo zinatumiwa na watu wengi wenye mafanikio
kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Njia hizo ambazo
zimethibitishwa na kutajwa na wataalamu mbalimbali wa mafanikio hasa baada ya
kuzitumia na kuona matokeo chanya ndizo hizo tunakwenda kuziangalia kupitia
makala haya.
Hebu twende pamoja tuangazie nukta kadhaa za kutusaidia
kujua njia zinazotumiwa na wengi kufikia mafanikio makubwa.
1. Maandalizi.
Kila wakati unahitaji
kujiandaa ili kufanikiwa. Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kuwa na
maandalizi mazuri. Ni lazima ujiandae kiakili na kimwili, ili ikusaidie
kukabiliana na kila changamoto unayokutana nayo.
Kwa mfano, wanamichezo
wote duniani kabla ya siku ya mashindano husika wanakuwa wana maandalizi
kwanza. Hakuna anayekwenda kushindana bila kujiandaa, kwa sababu wanajua maandalizi
hayo huwaandaa kushinda.
Hata kwenye maisha yako
ili uwe mshindi na kufikia kilele cha mafaniko ni lazima kujiandaa. Ni lazima
ujiandae kwa kuandika mpango wako nini ufanye na nini usifanye, changamoto za
kile unachataka kufanya ni zipi?
Tafuta njia sahihi ya mafanikio yako. |
Tambua ni lazima ujiandae
kufanya kazi kwa bidii na katika mazingira hata yale yaliyo magumu. Kile
ambacho umeamua kukifanya kifanye kwa nguvu mpaka kikupe mafanikio. Acha kupoteza
nguvu zako kwa kuishia katikati.
Unapokuwa na maandalizi
ya namna hii, hakuna kitakachokushtua sana hata ukipata matokeo usiyoyategemea.
Hivyo unaona kabisa kwamba, maandalizi ni njia mojawapo muhimu ya kukufikisha
kwenye mafanikio makubwa.
2. Kufanya kila siku.
Najua kuna kitu ambacho
umechagua kukifanya na unaamini kitu hicho kitakupa mafanikio, sasa kitu hicho
kifanye kila siku. Kitengenezee kitu hicho ratiba ya kukifanya kila siku yaani ‘daily routine’.
Haijalishi siku hiyo
umeamka unajisikia kukifanya au hujisikii kufanya kitu hicho, wewe fanya.
Usisikilize sauti ya mwili wako. Mafanikio hayawezi kuja kwa kufanya mambo kwa
kujisikia, yanakuja kwa kuchukua hatua za utendaji kila siku bila kujali hali
uliyonayo.
3. Kufanya kwa uhodari.
Ili kufanikiwa unahitaji
kutambua ni mambo yapi uliyobora na mambo yapi una udhaifu mkubwa ili
kurekebisha na kusonga mbele zaidi. Mafanikio yoyote yanatengenezwa kwa kufanya
mambo kwa uhodari na si kizembe.
Watu wengi wenye
mafanikio wanatumia njia hii ya kujiimarisha kila siku na hadi kuweza
kufanikiwa. Pale wanapokosea hujirekebisha, na kuzidi kufanya kwa ufanisi
mkubwa unaoleta mafanikio.
4. Maarifa.
Kati ya kitu ambacho kinakubaliwa
karibu na wataalamu wote wa mafanikio ni jinsi ya kuwa na maarifa bora. Maarifa
bora ni nguzo kubwa sana ya mafanikio yoyote duniani.
Ili uweze kufanikiwa ni
lazima uwe na maarifa bora. Utayapata maarifa haya kwa kujisomea na kujifunza
kwa wengine pia. Hii ni njia muhimu sana ambayo ukiitumia itakufikisha kwenye
kilele cha mafanikio.
Kabla sijafika mwisho wa
makala haya, inabidi uelewe kwamba maandalizi bora, kufanya kile unachokifanya kila
siku, kufanya kwa uhodari na maarifa ni njia mojawapo ambazo zinatumiwa na wengi
kufikiwa mafanikio makubwa.
Tunakutakia kila la kheri
katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kukaribisha
wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats
App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe. Hakuna gharama
na karibu sana.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.