google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 31, 2021

Kitu Hiki Kinaweza Kubadili Sana Maisha Yako, Ukikitumia Vizuri.

No comments :
Kuna wakati katika maisha unakuwa unajiona hali yako ni mbaya, au anakuwa unaona huwezi kupiga hatua tena na kila kitu kwenye maisha unakuwa unakiona kimeharibika na huwezi kupiga hatua za kukuwezesha kusonga mbele kimafanikio.
Kutokana na mambo yako kwenda hovyo, hakuna ambacho unakuwa unaona kina mafanikio kwako, zaidi ya kuona kushindwa kwingi sana. Inafika mahali unakata tamaa na kuamua kuharibu maisha yako zaidi na zaidi.
Ninasema unaharibu maisha yako zaidi na zaidi nikiwa na maana gani? Ni kwamba unakuwa umekata tamaa na unakuwa huchukui hatua yoyote ya maana sana sana unakuwa ni mtu labda wa kulewa sana au kuendesha maisha yako hovyo tu.
Kila ukiangalia sababu ya wewe kuweza kufanya yote hayo ni kwa sababu huoni tena mwanga wa mafanikio yako, bali unachikiona ni kushindwa na ambako unakuwa hujui hata wewe ufanyaje ili uweze kutoka hapo na kufanikiwa tena.
Hali kama hii inawakuta watu wengi sana, ambao kimsingi wanakua wanashindwa kuelewa ni nini cha kufanya kwa sababu ya hali zao mbaya za kiuchumi na badala ya kutengeneza maisha yao hujikuta ndio wanaharibu kabisa.

Ninachotaka kukwambia wewe hapa ni hiki, wakati wote hata kama hali ya maisha yako ni mbaya sana na unaona kila kitu kimeharibika, lakini kipo kitu ambacho unaweza ukafanya kikaleta mchango wa mabadiliko ya maisha yako.
Kitu hicho kinaweza kikawa na mchango mdogo sana ambao hauonekani kabisa, lakini kipo kitu cha kuweza kubadilisha maisha yako hata kama ni kwa kidogo sana. Unatakiwa kuthamini na kuchukua hatua za kutenda bila kujali kitu hicho ni kidogo au hapana.
Kama ilivyo kipo kitu ambacho ukifanya kinapelekea kuharibu maisha yako pasipo wewe kujua, halikadhalika kipo kitu ambacho ukikifanya kinaweza kubadili maisha yako ya kimafanikio hatua kwa hatua hata kama hatua hizo wewe huzioni.
Huhitaji kuendelea kukata tamaa zaidi ya hapo ulipo, kama ulikuwa umekata tamaa, inatosha kwa sasa, fanya kitu cha kuweza kubadili maisha yako. Usikubali kubweteka na kuwa mtu yule yule fanya kitu cha kubadili maisha yako na kitu hicho elewa kipo.
Unaweza ukaanza leo kuchukua hatua kwa kujenga ndoto zako upya ambazo unaona zimeharibika kabisa kwa kufanya kitu kidogo kabisa. Kitu hicho usikidharau na kukiona hakifai, kina mchango wake katika kukusaidia kukufanikisha wewe.
Mafanikio makubwa mara nyingi yanajengwa pia hivyo, kwa kufanya vitu vidogo vidogo ambavyo vitu hivyo kwa baadae vinakuja kuwa vina mchango mkubwa wa kuweza kubadili maisha kwa sehemu kubwa.
Je, bado una sita sita kuchukua hatua, je, bado unajiona huwezi tena kufanikiwa? Tafadhari usiogope, wala usizuiliwe na chochote kile. Chukua hatua kwa kufanya kitu kidogo sana ambacho kitakusaidia bila hata wewe kujua.
Fanyia kazi kitu hicho na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0687449428, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,








No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.