Jun 27, 2015
Kilimo Bora Cha Bilinganya.
Bilinganya imo
katika jamii ya
mimea inayohusisha nyanya,
pilipili, viazi mviringo
na nyanya mshumaa.
Mboga hii ina
viini lishe muhimu kama
vile madini aina
ya chokaa na
chuma, Vitamini A,
B na C,
wanga, protini na
maji. Mboga hii
hutumika kutengeneza supu
au kama kiungo
katika vyakula mbalimbali.
Vilevile huweza
kuhifadhiwa kwa kukatakata
vipande na kuwekwa
kwenye makopo.
MAZINGIRA:
Zao hili huhitaji hali
ya joto la wastani,
udongo wenye kina
kirefu na rutuba
ya kutosha na
usiotuamisha maji. Kwa
kawaida bilinganya hulimwa
zaidi ya msimu
mmoja, lakini katika
nchi za Kitropiki
(joto) zao hili
hulimwa kwa msimu
mmoja.
AINA:
Aina za
bilinganya zinazolimwa kwa
wingi katika nchi
za ukanda wa
joto ni kama
zifuatazo;-
·
Black Beauty:
Aina hii
huzaa sana, matunda
yake meusi, makubwa,
na ya mviringo
·
Florida Market.
Matunda ya
Florida Market yana
umbo la yai.
Aina hii pia
huzaa sana, lakini
hushambuliwa kwa urahisi
na ugonjwa wa mnyauko bakiteria
(Bacterial wilt)
·
Florida High
Bush.
Matunda yake
ni makubwa yenye
umbo la yai
na rangi ya
kijani kibichi iliyochanganyika na
nyeusi.
·
Newyork
Spineless.
Matunda ya
Newyork Spineless ni
ya mviringo, makubwa
na yana rangi
ya ya zambarau.
·
Peredeniya.
Aina hii
huzaa sana, matunda
yake ni makubwa
kiasi na yana
umbo la yai.
Aina zingine
za bilinganya ni
matale, Kopek na
Rosita. Aina hizi huvumilia
sana mashambulizi ya
ugonjwa wa mnyauko
bacteria.
KUOTESHA MBEGU:
Mbegu huoteshwa kwanza
kwenye kitalu na
baadaye miche huhamishiwa shambani. Kabla
ya kusia mbegu,
tengeneza tuta lenye
upana wa mita moja
na urefu wowote. Weka mbolea
za asili kama
vile samadi au
takataka zilizooza vizuri,
kiasi cha ndoo
moja au mbili
katika eneo la
mita mraba moja.
Sia mbegu kiasi
cha gramu mbili
mpaka tatu (nusu kijiko
cha chai chenye
ujazo wa gramu
tano) katika eneo
hilo.
Gramu 500
za mbegu zinatosha
kupandikiza katika eneo
la hekta moja.
Nafasi kati ya
mstari na mstari
iwe sentimeta 10
hadi 15 na
kina kiwe sentimita
1.5. Baada ya
kusia mbegu fukia
na tandaza nyasi
kavu na kisha
mwagilia maji. Endelea kumwagilia
kitalu kila siku,
asubuhi na jioni,
hadi mbegu zitakapoota. Mbegu
huota baada ya
siku ya 10 hadi 12.
KUHAMISHA MICHE:
Miche huwa
tayari kwa kupandikizwa
shambani baada ya
wiki sita hadi
nane. Wakati huu
huwa na urefu wa
sentimita 15 mpaka
20 (sawa na
urefu wa kalamu
ya risasi).
Mwezi mmoja
kabla kupanda miche, rutubisha
udongo kwa kuweka
mbolea za asili
zilizooza vizuri. Mbolea
hizi ni kama
samadi, mbolea vunde
na mbolea ya
kuku.
Weka kiasi
cha tani 10
hadi 20 kwa
hekta. Kiasi hiki ni sawa
na kuweka ndoo
moja hadi mbili
zenye ujazo wa lita
20 katika eneo
la mita mraba
moja. Mbolea ya
mchanganyiko aina ya
N.P.K yenye uwiano
wa 20:10:10 huwekwa
kwenye shimo wakati
wa kupandikiza mche.
Kiasi kinachohitajika ni
gramu tatu hadi
tano (sawa na
nusu kijiko mpaka
kijiko kimoja kidogo
cha chai) kwa
kila shimo.
Nafasi ya
kupandikiza hutegemea aina
ya bilinganya. Aina ndogo
hupandikizwa katika nafasi
ya sentimita 80
mpaka 100 kutoka mstari hadi
mstari na sentimita
50 mpaka 60
kutoka mche hadi
mche. Aina kubwa
hupandikizwa katika nafasi
nafasi ya sentimita
80 mpaka 100
kutoka mstari hadi
mstari na sentimita 80
mpaka 90 kutoka mche
hadi mche. Kazi
ya kuhamisha miche
ifanyike kwa uangalifu
mkubwa ili kuepuka
kuikata mizizi.
KUTUNZA SHAMBA:
·
Kuweka
matandazo.
Mara baada
ya kupandikiza miche,
tandaza nyasi
kavu. Matandazo husaidia
kuhifadhi unyevu, huzuia
magugu yasiote na
huongeza rutuba ya
udongo.
·
Palizi.
Hakikisha shamba
ni safi wakati
wote ili kuzuia
ushindani wa chakula,
maji na mwanga
kati ya mimea
na magugu. Usafi
wa shamba pia
huondoa maficho ya
wadudu waharibifu na
huzuia kuenea kwa
magonjwa.
·
Mbolea.
Mbolea ya
kukuzia aina ya
S/A huwekwa wiki
tatu baada ya
mmea kuanza kutoa
maua. Kiasi cha
gramu tatu hadi
tano kuwekwa kuzungukia kila
mche. Mbolea iwekwe
katika umbali wa
sentimita tano mpaka
15 kutoka kwenye
shina, hutegemea ukubwa
wa mche. Hakikisha
mbolea haigusi mmea.
·
Kukata kilele.
Wiki mbili
baada ya kupandikiza miche,
kata sehemu ya
juu ya mmea (kilele)
kama umepanda aina
ndefu ya bilinganya.
Hii itasaidia kupata
matawi matatu hadi
manne na mmea
kutengeneza kupata matawi
matatu hadi manne
na mmmea kutengeneza
umbile la kichaka.
Matawi yakizidi manne
yaondolewe ili kupata mazao
mengi na bora.
·
Kumwagilia.
Zao la
bilinganya hustawi vizuri
likipata maji ya
kutosha. Umwagiliaji ufanyike
kila siku asubuhi
na jioni kutegemea
hali ya hewa.
Kuzuia Wadudu
Waharibifu na Magonjwa.
Wadudu Waharibifu:
·
Vivyatomvu wa
Bilinganya (Eggplant Lacebugs)
Wadudu hawa
hushambulia zaidi
sehemu ya chini
ya jani. Hufyonza
utomvu wa majani na
kusababisha majani kuwa
na mabaka meupe
au njano. Mashambulizi yakizidi
majani huanguka chini.
Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa
kwa kunyunyizia moja
ya dawa zifuatazo;-
Deltamethrin (Decis), Dimethoate (Sapa
Dimethoate) Fenvalerate
(Sumicidin), Lambda -
Cyhalothrin (Karate).
·
Vidukari au
wadudu mafuta (Cotton
Aphids)
Hawa ni
wadudu wadogo wenye
rangi nyeusi. Hushambulia majani
machanga na kuyasababisha kudumaa
na kukunjamana. Zuia
wadudu hawa kwa
kutumia mojawapo ya
dawa zifuatazo;-
Dimocron 50%
E.C, Lambda - Cyhalothrin
(Karate) Dichlorvos (Nogos).
·
Utiriri wa
Mimea (Red Spider
Mites).
Ni vidudu
vidogo vyenye rangi
nyekundu iliyoiva.
Hushambulia majani kwa
kufyonza utomvu. Majani
yaliyoshambuliwa huonyesha utando
kama wa buibui.
Mashambulizi yakizidi mea
hudumaa, majani hukauka
na hatimaye hufa.
Utiriri unazuiwa
kwa kutumia dawa
zifuatazo;- Acrex, Karathane 25% W.P,
Dimethoate, Ekalux, Kelthane.
·
Minyoo Fundo
(Root knotnematodes).
Wadudu hawa
hushambulia mizizi. Hutoa
kinyesi ambacho ni
sumu kwa mmea.
Sumu hii husababisha
mizizi kuwa na
nundu kama ya
mizizi ya maharagwe.
Mashambulizi yakizidi mmea
hudumaa, hunyauka na
hatimaye hufa.
Njia ya
kuzuia wadudu hawa
ni kubadilisha mazao
kwa mfano baada
ya kuvuna zao
hili, zao linalofuata
lisiwe la jamii
moja na bilinganya
kama vile nyanya,
pilipili na viazi
mviringo. Pia dawa
aina ya Carbofuran
(Furadan) inaweza kutumika.
Magonjwa:
·
Mnyauko Bakteria
( Bacterial Wilt).
Ugonjwa huu
husababishwa na backteria.
Mmea ulioshambuliwa hunyauka
ghafla hasa wakati
wa jua kali.
Mnyauko bacteria
unaweza kuziuwa kwa
kubadilisha mazao shambani.
Endapo ardhi itashambuliwa na
ugonjwa huu zao
la bilinganya lisipandwe
katika eneo hilo
kwa muda wa
miaka mitatu hadi
mitano.
Njia nyingine
ni kupanda aina
za bilinganya kama
vile Matale, Kopek
na Rosita ambazo
huvumilia mashambulizi ya
ugonjwa huu.
·
Phomopsis Vexans:
Ugonjwa huu
husababishwa na bacteria
na kushambulia majani,
shina na matunda.
·
Verticillium Wilt.
Huenezwa na
maji na husababisha mmea
kudumaa, majani kukunjamana
na kuanguka.
Magonjwa ya
Phomopsis vexans na
Verticillium Wilt yanaweza
kuzuiwa kwa kung’oa
ma kuchoma moto
mimea iliyoshambuliwa, kubadilisha
mazao, na kuweka
shamba katika hali
ya usafi wakati
wote.
KUVUNA:
Bilinganya huanza
kutoa matunda yaliyokomaa
baada ya miezi
miwili hadi mitatu
tangu kupandikiza. Uvunaji
huendelea kwa muda
wa zaidi ya
miezi minne na
hauna budi ufanyike
mapema mara matunda
yanapokomaa. Matunda yaliyokomaa sana
hayafai kulimwa kwa
sababu huwa na
kambakamba na mbegu
zilizokomaa.
Vuna mara
mbili au tatu
kwa wiki, kwa
kutumia kisu kikali
ili usiumize matunda.
MAVUNO:
Kwa kawaida
zao hili huzaa
sana iwapo limetunzwa
vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri
linaweza kutoa mavuno
tani 50 hadi
60 kwa hekta.
Hata hivyo mavuno
mengi hutegemea aina
ya bilinganya, umwagiliaji na
rutuba ya udongo.
§ MAKALA HII IMEANDALIWA NA SAID MALOGO,
MTAALAMU WA MASUALA YA KILIMO.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.