Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, February 17, 2016

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuitengeneza Tabia Yako Kabla Tabia Yako Haijakutengeneza Wewe.

No comments :
Tabia ni mazoea yaliyopitiliza kiwango cha kawaida. Ni mazoea yaliyozidi kawaida. Mazoea yakizidi katika kufanya jambo lolote ndio hujenga tabia. Kwa maana hiyo basi tunapata ukweli kuwa tabia njema au mbaya tunatengeneza wenyewe kutokana na mazoea. Kuwa na tabia njema au mbaya ni uamuzi wa mtu binafsi katika kuamua kuacha au kuendelea kufanya kitu chenye kujenga au kubomoa na kuharibu kabisa tabia yake.

Kwa mfano ukizoea kunywa kunywa mwisho utakuwa mlevi. Ukizoea kuibaiba mwisho utakuwa mwizi. Ukizoea kusomasoma utakuwa msomaji mzuri. Ukizoea  kulimalima utakuwa mkulima. Mazoea yanajenga Tabia. Hivyo ukitaka kufanikiwa ni maamuzi yako na ukitaka kutofanikiwa pia ni maamuzi yako.

Kila unachofanya katika maisha yako kitakupa matokea halisi ya kile unachofanya haijalishi ni matokeo hasi au chanya. Ndio maana wataalamu wa saikolojia tunasema ukitaka kujua tabia ya mtu mwambie akuonyeshe marafiki zake. Huu ni ukweli wa asilimia mia moja. Huwezi kuwa na marafiki walevi  wewe usinywe, utakuwa jiniazi kama mzee wa nyundo. Huwezi kuwa na marafiki wahuni nawe usalimike ngumu utashawishika tu.

TENGENEZA TABIA ZA MAFANIKIO.
Ukikaa na ua waridi nawe utanukia, ukikaa na wasomi nawe utaelimika, ukikaa na watu wenye ‘vision’ nawe utabalika. Hapo ndipo tunaposema binadamu mafanikio yake ni jumla ya watu watano anao amka nao, kushinda nao na kulala nao ‘that's all about success’.

Maisha ya mafanikio ni rahisi leo nakuibia siri.

1.Tambua uwezo wako katika kufikiri na kutenda.

2.Tambua kipawa/kipaji chako.

3. Kuwa mkweli na muwazi.

4. Chagua marafiki wa kwenda nao sambamba wenye malengo na maono yanayofanana na yako.

5. Jiamini kuwa unaweza kama mimi navyojiamini. Leo mtu ukimwambia leo toa somo atakuambia siwezi, wewe nani alizaliwa anaongea na kujua majina ya vitu?

6. Kuwa na ‘network’ ya watu wazuri unao link nao katika kutafuta mafanikio.

7. Jenga tabia ya kutopoteza muda wako bure kwa vitu vya kipuuzi ambavyo havina faida katika maisha yako.

8. Kuwa na ratiba katika kufanya vitu vyako.

9. Kuwa na bajeti na nidhamu katika matumizi yako ya pesa.

10. Ondoa Hofu katika mambo unayofanya .

11. Kuwa na vipaumbele katika maisha yako. Na vipaumbele viko vya aina 6 tutajifunza mbeleni katika masomo yajayo.

Kwa leo naomba tuishie hapa na ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Endelea kuwasharikisha wengine waweze kufaidi na makala tunazotoa hapa.

Ni wako rafiki katika kuyasaka mafanikio ya kweli,

Shariff Kisuda aka Mzee wa Nyundo Kali,
Simu0715 079 993,
Blogdirayamafanikio.blogspot.comNo comments :

Post a Comment