Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, February 12, 2016

Kushindwa Kupanga, Ni Kupanga Kushindwa.

No comments :
Katika maisha hakuna kitu chenye thamani kama kuwa na mipango imara yenye kutekelezeka kila siku. Ili ufanikiwe katika maisha ni lazima uwe na mipango, bila ya mipango hakuna mafanikio katika maisha yako kabisa. Mipango ya maisha ndiyo dira na mwongozo wa mtu katika kuyafikia mafanikio na maisha mazuri.
Mtu mwenye mipango huwa na malengo katika  maisha yake. Mtu mwenye malengo huishi maisha ya ndoto yake. Mtu mwenye malengo hapangiwi maisha yake hujituma yeye mwenyewe. Mtu asiye na mipango ni mtumwa wa maisha yake.
Kukosea kupanga ni kupoteza ndoto zako na kutimiza ndoto za wenzio waliopanga mipango ya maisha yao. Kwa nini watu wanashindwa kupanga maisha yao? Na kwa nini wengine wameweza kupanga mipango yao katika maisha na kutimiza ndoto zao? 
Sababu kuu ya kuweza au kushindwa kupanga mipango katika maisha iko katika KUFANYA MAAMUZI. Maamuzi yako ndio huamua kupanga kwako au kushindwa kupanga ktk Mipango yako ya maisha. Leo naomba nikupe njia 10 nzuri za kufanya kabla ya kufanya maamuzi na mipango yako ktk maisha:-

Kushindwa Kupanga, Ni Kupanga Kushindwa.
JIWEKEE MALENGO.
1. Usifanye haraka katika kutoa maamuzi.
2. Jipe muda wa kutosha kufikiri kabla ya kutoa maamuzi.
3. Lipime na kulitazama jambo kwa marefu na mapana kabla ya kutoa maamuzi.
4. Tafuta ushauri kwa wataalamu.
5. Tumia makosa yako ya nyuma kama njia ya kujifunza.
6. Sikiliza Hisia zako yaani sauti yako ya ndani.
7. Usitoe maamuzi ukiwa na hasira.
8. Angalia ni nini makusudio ya maamuzi yako.
9. Chunguza ni nini athari za maamuzi yako.
10. Jielewe udhaifu wako na mapungufu yako katika kufanya maamuzi yako.
Asante kwa kutembelea na kufuatilia blog yetu waalike na wengine ili wafaidike na makala  tunazotoa hapa.

Makala hii imeandaliwa na Shariff H. Kisuda a.k.a Mzee wa  Nyundo Kali.
Simu; 0715-079993
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment