Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, February 10, 2016

Kama Unatafuta Mafanikio Makubwa, Huwezi Kukwepa Maumivu.

No comments :
Mabadiliko makubwa ambayo unayahitaji katika maisha yako kuna wakati huwa hayaji kirahisi tu kama tulivyozea, ila huja na kuambatana na maumivu. Maumivu haya ambayo unakuwa unayapata wakati mwingine hupelekea hata kujiona kama umekosea ndoto zako na usipokuwa makini unaweza kuachana na kile unachokifanya katika maisha yako.
Jaribu kuangalia kile kipindi ambacho ulikuwa umejiwekea malengo yako makubwa na ambapo ulitakiwa kujizuia na baadhi ya mambo ili malengo yako yatimie, ni nini ambacho kilitokea? Bila shaka uliumia sana kwa kuona unajikosesha raha ya kuishi au umekosa uhuru fulani hivi.
Lakini si hivyo tu hata wale rafiki zako uliokuwa nao na ambao mlikuwa mna malengo yanafanana wengine waliachana na wewe na kuamua kuishi maisha yao ya kawaida na kusahau kwamba siku zote mafanikio makubwa yanapatikana kwa maumivu.
Jiulize umeacha malengo mangapi mazuri kwa sababu ya maumivu ambayo umekuwa ukiyaona yatakulemea kwa sababu ya mabadiliko unayotaka kufanya? Bila shaka ni mengi. Hapo ndipo ulipokuwa ukikosea zaidi ulishindwa kutambua kwamba siku zote mafanikio yanakuja kwa maumivu.

Kama Unatafuta Mafanikio Makubwa, Huwezi Kukwepa Maumivu.
MAUMIVU NI SEHEMU YA KUKUSAIDIA KUFIKIA LENGO
Ili uweze kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa unayoyataka, hii ni kanuni ambayo hutakiwi kuikwepa, lazima uitekeleze. Kipo kipindi katika maisha ambacho unatakiwa kuacha karibu kila kitu ikiwa pamoja na familia, usingizi, kuachana na marafiki kwa muda na kuacha mambo mengi matamu kwako kwa sababu ya mafanikio.
Bila kufanya hivyo au kuachana na mambo hayo kwa muda inakuwa ni ngumu kufikiwa mafanikio makubwa, zaidi unaweza ukawa ni mtu wa mafanikio madogo na ya kawaida sana. Naamini hata ukifatilia watu wengi waliofanikiwa walifanya hivi na kuachana karibu na kila kitu ili kutimiza malengo yao.
Hivyo kitu cha kutambua hapa ni kwamba maumivu ni muhimu wakati mwingine ili kufikia mafanikio yetu makubwa. Tatizo kubwa linalowakabili binadamu wengi ni ule uasili wa kukataa mabaliko. Mara nyingi unapotaka kufanya kitu fulani nje ya kile ulichokizoea mwili huwa unapiga kwelele sana.
Kama unafikiri natania jaribu kuamka asubuhi na mapema kuliko kawaida yako uone nini kitatokea. Mwili utakataa sana. Hali hiyo huja kwetu, nakuona kama maumivu fulani ambayo hatujayazoea ambayo hutupelekea kuweza kukata tamaa au kuacha kabisa kile tunachokifanya kwa mawazo ya kuona kama tunajitesa.
Lakini kwa kuwa siku ya leo umeujua ukweli huu, tambua wakati mwingine mafanikio yanakuja kwa maumivu. Inatakiwa ulitambue hilo na kuacha kukubaliana sana na kile ambacho mwili wako unakwambia sana. kwa kufanya hivi utakuwa unajitengenezea mazingira mazuri ya mafanikio yako.
Kama kuna jambo unalifanya lifanye tu. Hata kama kuna wakati unajihisi umechoka, unajihisi mwili unapiga kelele kama unaumia, jipe muda wa kuvumilia. Hayo kwako ni mapito tu. Na mafanikio makubwa yoyote duniani mara nyingi huwa yanapatikana kwa namna hiyo. Endelea kusonga mbele utafanikiwa.
Nikutakie siku njema na endelea kutembelea mtandao wetu wa DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza na kuhamsika. Waalike na wengine ili waweze kufaidika na mafundisho mazuri yanayoendelea hapa.
Ni wako rafiki, 
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment