Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, February 3, 2016

Usikubali Jambo Hili Dogo Likuzuie Kufikia Mafanikio Yako.

No comments :
Moja ya tabia kubwa waliyonayo watu wenye mafanikio, ni tabia ya kuhoji au kujiuliza mara kwa mara ndani ya nafsi zao. Mara nyingi huwa si watu wa kukubali kirahisi kila hali inayotokea maishani mwao, hawa huwa ni watu ambao hutaka sana maelezo kwenye majibu yanayotolewa.
Hawa si aina ya watu wanaoridhika tu na kile wanachoambiwa katika maisha yao, bali ni watu wa kujiuliza kwa hali nyingi zinazojitokeza kwao. Hujiuliza sana juu maisha yao kwa nini yako hivyo, na pia hujiuliza kwa mambo mengine yanayotokea kwenye maisha yao kwa ujumla.
Maswali haya ambayo hujiuliza siku zote yanawasaidia kuweza kuboresha maisha yao kwa namna moja au nyingine. Yanakuwa ni maswali ya udadisi ambayo yanawapa nguvu ya kufanya zaidi ya kile wanachokifanya. Na pia ni maswali yanayowasaidia kuwapa majibu mengi kwa yale wasiyoyajua.
Lakini hata katika hali ya kawaida ili uweze kufanikiwa unatakiwa kujifunza sana kujiuliza au kudadisi  na kutokuwa mwepesi sana wa kukubali kila kitu. Unapokubali kila kitu bila kuhoji uhalali au sababu ya kitu  hicho wengi watakupoteza na kujikuta umefanya mambo mengi kwa njia ambayo si sahihi kwako.

TAFUTA NJIA YA KUFANIKIWA.
Kwa jambo lolote unalotaka kujiingiza au kulifanya ni vyema ukajiuliza maswali mengi hata kama maelezo yake unaona yako sawa. Sio dhambi kujihoji hata wewe mwenyewe ndani yako, ikiwa utashindwa hadharani. Hakuna ulazima wa wewe kupokea jambo kama lilivyo na kukubaliana na kila kitu.
Acha kujiendelezea wepesi wa kukubali kila jambo kwa haraka. Unapoambiwa kitu kama kinagusa maisha yako jifunze kuhoji ndani mwako kwanza kabla hujatoa maamuzi. Vinginevyo ikiwa utakuwa unatoa maamuzi bila kujihoji upo uwezekano mkubwa wa kujuta baadae.
Hata pale inapotokea unatakiwa kutoa maamuzi kwenye kitu ambacho maelezo yake yanaonekana yapo sawa ni muhimu pia kujihoji juu ya jambo hilo. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu maamuzi utakayokwenda kuyatoa yatakuwa tayari yanathari kwenye maisha yako au mwingine.
Kama nilivyoanza kusema jifunze siku zote kujiuliza maswali yatakayokusaidia kuboresha maisha yako.  Jifunze kujiuliza maswali yatakayosaidia kuboresha maisha ya wengine pia wanaokuzunguka. Jifunze kuwa mdadisi wa mambo mengi sana ya kukusaidia.
Acha kujichelewesha kuyafikia mafanikio ya maisha yako eti kwa sababu ya kushindwa kujiuliza. Jiulize kila siku ‘kwa nini mimi niko hivi, kwa nini maisha yangu mabovu, nifanye nini ili nitoke hapa nilipo, ni boreshe kipi, ni tabia gani zinazoniangusha?’ Jiulize.
Kila siku endelea kujiuliza siku hadi siku. Jiulize juu ya maisha yako. Jiulize juu ya maisha ya wengine. Jiulize juu ya kila hali unayokutana nayo na tafutia majibu yake upesi. Kwa kujiuliza hivi utajikuta ukiboresha maisha yako na ya wengine bila kujua.
Hata siku moja usikubali jambo hili dogo likuzuie kufanikiwa. Hii ni kanuni rahisi sana ambayo unaweza ukaifanya ikawa sehemu ya maisha yako. Kwa udadisi utakao kuwa ukiujenga kila siku, utakupa nguvu ya kufanya mambo mengine ya ziada kwa kuboresha maisha yako zaidi na zaidi.
Nikutakie siku njema na kila la kheri katika safari ya mafanikio yako makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Simu0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
No comments :

Post a Comment