Feb 16, 2016
Mambo Muhimu Ya Kukusaidia Kukuza Biashara Yako Wakati Wote.
Kila
mfanyabishara mwenye nia ya kufikia mafanikio makubwa, lengo lake kubwa la
kwanza huwa ni kutaka kukuza biashara yake na kufikia mafanikio makubwa. Hakuna
mfanyabiashara ambaye anakua hana nia hii, kila mmoja hutamani kuona biashara
yake ipo sehemu fulani kimafanikio siku hadi siku.
Lakini
pamoja na juhudi nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa za kujitahidi kukuza
biashara, wengi hujikuta wakishindwa kufikia lengo hilo. Hapo ndipo huanza
kujiuliza tatizo ni nini? Leo katika makala yetu, nakushirikisha mambo muhimu
ya kukusaidia kukuza biashara yako wakati wote.
Karibu
sana na twende pamoja kujifunza mambo hayo ili yawe msingi mkubwa katika kukuza
biashara yako;-
1. Toa huduma bora.
Kama
hamu yako kubwa ni kuona biashara yako ikikukua kwa kasi, jifunze kutoa huduma
bora kabisa na sio bora huduma. Kama hutabadilika na ukaendelea kutoa huduma
mbovu, sahau kabisa biashara yako kukua. Utaendelea kubaki hapohapo. Siri kubwa
ya kukuza biashara yako, hakikisha unatoa huduma bora siku zote bila kuacha.
TENGENEZA VYANZO VINGI VYA FEDHA. |
2. Toa bidhaa zenye ubora mkubwa.
Njia
bora kabisa itakayokusaidia kukabiliana na ushindani na kukuza biashara yako,
ni kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Kama utakuwa unatoa bidhaa zina
ubora wa hali ya juu popote pale utakapokuwepo ni lazima wateja wako wakufuate.
Tumia muda wako mchache, kutafiti namna ambavyo unaweza ukatoa bidhaa bora
kabisa itakayomridhisha mteja wako.
3. Jifunze kuwa na lugha nzuri.
Unaweza
ukawa una huduma iliyobora na unatoa bidhaa bora, lakini kama huna lugha nzuri
kwa wateja hiyo itakuwa ni sumu kubwa sana kwenye biashara. Kwa vyovyote vile
iwavyo lugha nzuri, ni kitu muhimu sana kwenye biashara ambacho kinauwezo
wakukusaidia kukuza biashara yako nyakati zote.
4. Jali muda wa wateja wako.
Muda
siku zote ni mali. Ukipotea umepotea. Kama ni hivyo ili kijipa uhakika wa
kukuza biashara yako, jifunze sana kujali muda wa wateja wako. Fanya chochote
kile ufanyacho kulinda muda wa mteja usipotee hovyo. Usimpotezee mteja muda
wake bila sababu. Hii ni njia mojawapo
bora sana itakayokusaidia kukuza biashara yako. Bila kufanya hivyo utapoteza
wateja wengi sana.
5. Kuwa na punguzo maalum la bei.
Katika
biashara yako acha kuacha bei ikawa juu kila wakati. Kuna wakati unatakiwa
kuonyesha kwa wateja wako kuwajali zaidi kwa kuwawekea punguzo maalumu la bei. Hiki
ni kipindi kinaweza kikawa cha sikuu au wakati maalumu ambao wewe utaamua. Hiyo
itawapa hamasa kubwa sana wateja wako kuvutika na biashara yako.
6. Weka matangazo.
Matangazo
ni kitu cha muhimu sana katika ukuaji wa
biashara yoyote. Itangaze biashara yako kupitia wateja wako hao hao ulionao.
Hiyo haitoshi, unaweza ukatengeneza vipeperushi vidogo vidogo vinavyoonyesha biashara
yako. Lakini kama mtaji unaruhusu unaweza ukaitangaza biashara yako kupia redio au televisheni.
Hiyo itakusaidia sana kukuza biashara yako eneo kubwa na kwa muda mfupi.
7. Boresha biashara yako mara kwa
mara.
Kwa
kawaida tunapofanya biashara huwa kuna mapungufu yale ambayo yanajitokeza.
Mapunguf haya unaweza ukayapata kutoka kwa wateja kwa njia ya malalamiko au
kutoa maoni yao moja kwa moja kwako. Inapotokea hivyo, fanya marekebisho ya
haraka mno bila kuchelewa. Ikiwezekana wawekee kisanduku cha maoni. Hiyo
itakusaidia kuza sana biashara yako na kuwa kubwa kuliko unavyofikiri.
Kwa
kifupi, hayo ndiyo mambo muhimu yanayoweza kukusaidia kuikuza biashara yako
wakati wote. Yafanyie kazi mambo hayo yatakusaidia sana kukuletea mabadiliko
makubwa katika bishara yako leo na kesho.
Nikutakie
siku njema na mafanikio makubwa katika biashara yako na endelea kuwashirikisha
wengine kujifunza kupitia mtandao wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni
wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu;
0713048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.