Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, November 8, 2016

Siri Ya Kujua Kanuni Za Asili Za Mafanikio.

No comments :
Kama ambavyo mara nyingi tumekuwa tukisema, maisha tunayoishi yanaongozwa na kanuni zake. Na kwa bahati mbaya au nzuri uwe unazijua au huzijui kanuni hizo, zinafanya kazi wakati wote katika maisha yako na zitakupa matokeo.
Na kila mtu ana uhuru wa kuchagua kutumia au kutotumia sheria za asili za mafanikio. Uchaguzi wowote utakao uchagua ni lazima ukupe matokeo, haijalishi ni chanya au hasi. Lakini, hakuna mtu ambaye ataweza kukwepa matokeo ya kutumia au kutotumia kanuni za mafanikio.
Kwa kujua umuhimu wa kanuni au sheria hizi katika mafanikio, tutaanza kujifunza baadhi ya kanuni za asili za mafanikio na kuona jinsi ambavyo zinasaidia kutufanikisha katika maisha yetu.
Watu wenye mafanikio wanatumia kanuni hizi za asili za mafanikio kuweza kuwafanikisha. Ni kanuni ambazo hazibagui, ni lazima zikupe matokeo iwe umezitumia au hujazitumia.

Kanuni hizi za mafanikio si wengi sana wanaozifahamu, ingawa zipo katika maisha yetu kila siku na zinatoa matokeo kila kukicha.
Mara nyingi ikiwa unaishi nje ya kanuni hizi, ni rahisi sana kuanza kuona maisha yako kama hayasogei kwa kiasi kikubwa. Kunakuwa kuna ugumu fulani hivi kwenye maisha yako, ambao hata wewe unakuwa hujui unatokana na nini.
Kwa hiyo, utakapojifunza na kuzijua sheria hizi na kuzitumia, utafurahia jinsi maisha yako yatakavyokuwa yakieenda kwa wepesi ambao hata hukitarajia mwanzoni.
Mambo ambayo yalikuwa yakikupa hasira sana, utashangaa hayakupi tena hasira.
Wasiwasi uliokuwa nao utashangaa ukipungua na kutoweka.
Woga wa mambo mbalimbali ikiwemo pamoja na kuthubutu pia utakutoka na kuwa mtu wa vitendo.
Hata pia utaweza kujihakikishia mafanikio makubwa, ikiwa utazifanya sheria hizi kuwa sehemu ya maisha yako.
Hayo yote yatatokea si kwa bahati mbaya wala muujiza, bali ni kwa sababu sheria au kanuni za mafanikio zinakuwa zipo kazini.
Kanuni hizi, ambazo tutakwenda kuziangalia moja baada ya nyingine yaani kanuni za asili za mafanikio, ni vyema tukajua nini maana yake? Yaani Tunapozungumzia kanuni za asili za mafanikio tunamaanisha nini?
Kanuni za asili ni mfumo au taratibu unaoendesha maisha bila kufuata taratibu za jamii yoyote. Mfumo au utaratibu huu upo wakati wote, ni mfumo ambao upo kama kiroho, ni mfumo ambao hauonekani kwa macho haya, lakini unafanya kazi vizuri tu, ndio maana zinaitwa kanuni za asili za mafanikio yaani ‘Universal Laws’.
Kwa hiyo, tutaanza kujifunza kanuni mbambali za mafanikio kadri muda utakavyoturuhusu. Kati ya kanuni za asili za mafanikio tutakazokwenda kuzangalia ni pamoja na kanuni ya asili ya karma, kanuni ya asili ya kusamehe, kanuni ya asili ya uvutano na nyinginezo nyingi.
Kwa leo tuishie hapa, tukutane wiki lijalo siku kama hii ya leo, kuanza kuangalia kanuni moja baada ya nyingine ili zikupe msingi mkubwa wa mafanikio yako.
Nakutakia kila la kheri na ushindi katika kufikia mafanikio yako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki,

IMANI NGWANGWALU,No comments :

Post a Comment