Nov 14, 2016
Tabia Unazotakiwa Kuzijenga Pale Unapokuwa Na Fedha.
Katika
hali ya kawaida, ili uweze kupata pesa na zikadumu mikononi mwako, zipo tabia
ambazo ni lazima uwe nazo. Ni ngumu sana kuendelea kuwa na pesa kama huna tabia
hizo ambazo ni kama msingi wa kukupa pesa zaidi.
Watu
wengi maisha yao yamekuwa hovyo, kwa sababu ya kukosa tabia hizi. Utakuta mtu
anapata pesa leo, ukionana nae kesho, pesa hizo hana, haya yote hutokea kwa
sababu ya kukosa tabia hizo za msingi.
Ikiwa
nia yako unataka kutengeneza pesa za kutosha na hata zile pesa ulizonazo ziweze
kudumu, ni muhimu na lazima kuendeleza tabia hizi ambazo tunakwenda kuzijadili
katika makala haya.
Hebu
twende nami pamoja kujifunza kupitia makala haya, nikuonyeshe tabia unazotakiwa
kuzijenga hasa pale unapokuwa na pesa.
1. Tabia ya kuweka akiba.
Kuweka
akiba ni jambo la muhimu sana katika mafanikio ya mjasirimali. Uwe unataka au
hutaki ni lazima sana kwa mjasirimali anayetaka mafanikio, kujifunza kujiwekea
akiba kila wakati.
Zipo
faida nyingi zitokanazo na kujiwekea akiba, ikiwa pamoja na kusaidia katika
suala zima la kuwekeza pesa hizo zinapokuwa nyingi. Pia kujiwekea akiba
inakusaidia kujenga msingi imara wa kipato chako.
Ni
lazima uweze kujiwekea akiba kwa kiasi chochote cha pesa unachopata. Kila
unapopata pesa anza kwanza kuweka akiba, kisha inayobaki tumia. Hii ni siri
kubwa inayotumiwa na watu wote wenye mafanikio ya kifedha duniani.
2. Tabia ya kuweka vipaumbele juu ya
matumizi yako.
Ili
uweze kujijengea kipato cha kudumu, unalazimika kuweka vipaumbele juu ya
matumizi yako. Vipaumbele hivi unavyokuwa unaweka vinakusaidia kujua, kipi
ununue na kipi usinunue na pesa zako.
Kitendo
cha kuwa makini na pesa zako, hadi kujua kipi cha muhimu na kipi si cha muhimu
kwa sasa, hiyo itakuwa ni ishara tosha kwamba sasa unaweza kuitawala pesa, na
si pesa ikutawale wewe.
Kuweka
vipaumbele kwenye matumizi yako, ni njia mojawapo bora ya kukufanya ukawa ni
mjasiriamali mwenye mafanikio. Unapokuwa na pesa muda wote, hakikisha unakuwa
mtu wa kuweka vipaumbele, acha kupuuza juu ya hilo na utafanikiwa sana.
3. Tabia ya kuandika matumizi yako ya
pesa.
Hautaweza
kujua sana pesa zako zinatumikaje, ikiwa hauziwekei kumbukumbu. Mbinu ya
kukusadia kujua hili vizuri, ni kuandika kila aina ya matumizi unayofanya.
Hutakiwi kudharau juu ya hili kila kitu ni lazima uandike.
Kuna
msemo usemao, ‘mali bila daftari hupotea
bila habari,’ hivyo kwa kujua hili, nunua kijitabu chako cha mtumizi na
kuandika kila aina ya shilingi ambayo unaitumia kwa siku.
Utafika
mbali kimafanikio ikiwa utaikumbatia tabia hii na kuwa yako. Hiyo inakuwa hivyo
kwa sababu kila matumizi yanapokuwa juu, inakuwa sawa kama una alamu
inayokwambia punguza matumizi. Ishi kimafanikio kwa kuandika kila aina ya
matumizi yako.
4. Tabia ya kuwekeza.
Huwezi
kuendelea ukawa una pesa, kama kila pesa unayoipata unatumia yote. Upo umuhimu
mkubwa sana wa kuwekeza angalau sehemu kidogo ya pesa yako unayoipata ili
ikusaidie kuzalisha.
Pengine
unajiuliza, sasa kama pesa ninayopata ni kidogo ninaanzaje hapo kuwekeza? Jibu ni
rahisi tu, anza kwa kuweka akiba kwanza. Akiba yako itakapokwa nyingi itaenda
kwenye uwekezaji moja kwa moja unaoutaka.
Kimsingi,
ili uweze kutengeza kipato cha kudumu, kipato ambacho kitakuwa endelevu leo na
kesho, ni vyema ukajifunza kujenga tabia hizo na zikawa za kudumu kwako wakati
unapokuwa na pesa.
Chukua
hatua na endelea kubadili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi za mabadiliko,
kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Nikutakie
siku njema na mafanikio mema.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.