google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 4, 2016

Matatizo Yanayosababishwa Na Kuahirisha Mambo.

No comments :
Kuahirisha mambo, ni jambo ambalo hufanywa sana na karibu kila mtu katika maisha yake. Utakuta kitu ambacho kilitakiwa kifanyike leo, kinasogezwa mbele hadi kesho au siku nyingine.
Hali hii huonekana ni kitu cha kawaida na yamekuwa mazoea ya wengi kuahirisha mambo bila sababu yoyote ile. Kwa bahati mbaya sana, pamoja na wengi kuahirisha mambo yao, lakini hata hivyo wanakuwa hawajui madhara makubwa yatakanayo na kuahirisha mambo.
Moja ya madhara makubwa yanayosababishwa na kuahirisha mambo  ni msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unakuja kutokea hasa pale kazi ambayo ulitakiwa kuikamilisha mapema sasa inakuwa inahitajika.

Kwa mfano, unaweza ukawa umeajiriwa na bosi wako akakupa kazi fulani. Ukishindwa kuifanya kazi hiyo kwa muda na kuahirisha sana, siku ikitakiwa ni lazima utapata msongo wa mawazo na kujiuliza sana ufanyaje ili kazi hiyo ikamilike.
Mbali na msongo wa mawazo tatizo lingine ambalo unaweza ukakumbana nalo kwa sababu ya kuahirisha mambo yako ni kupoteza furaha. Hauwezi kuwa na furaha hata kidogo kama kitu ulichotakiwa kukamilisha, hakijakamilika na kinatakiwa kwa kwa haraka.
Ni lazima ndani yako utakuwa na wasiwasi mwingi kwamba jambo hili au kazi hii haijakamilika na muda umekwisha sasa hapo nafanyaje fanyaje? Maswali mengi kama hayo ni lazima yatakupotezea furaha yako ya moja kwa moja.
Pia ikiwa utakuwa unaahirisha mambo mengi sana, upo uwezekanao mkubwa wa wewe Kutokufanya kazi zako kwa kwa usahihi. Kazi nyingi ambazo mara nyingi zinafanywa muda ukiwa umebaki kidogo huwa hazifanyiki vizuri, zinakuwa ni kazi za kulipua lipua.
Kwa kifupi, hayo ndiyo matatizo yanayosababishwa na kuahirisha mambo mara kwa mara katika maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafikio.blogspot.com kila siku.
 Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,




.



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.