google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 15, 2016

Sheria Ya Mafanikio; Unapokea Kile Unachotoa.

No comments :
Maisha ya binadamu ni matokeo ya kile alichopanda au kukitoa katika maisha yake siku za nyuma. Haijalishi upo katika hali ya mafanikio au kushindwa, haijalishi pia upo katika hali ya afya au ugonjwa, yote hayo ni matokeo ya ulichopanda.
Sheria ambayo inapelekea yale tuliyoyatoa au kuyapanda kurudi kwetu tena, sheria hii inafahamika kama ‘Karma’ au ‘law of karma’. Ni sheria ya asili, ambayo inaonyesha wazi kwamba kile unachokitoa, ni lazima utakipata.
Katika sheria hii ya asili, inasisitiza sana kwamba chochote akipandacho mtu, mfano wema, ubaya, upendo, ni lazima kitu hicho mtu huyo atakivuna iwe anataka au hataki.
Mwasayansi Isack Newton katika moja ya sheria zake aliwahi kusema, ‘every action must have reaction,’ Akiwa na maana kwamba katika kila tendo/hatua, upo mrejesho wake, haijali ni mbaya au mzuri.
Hapo utaona Isack Newton alitoa kitu kilekile kinachofanana na sheria ya asili ya ‘karma’ kwamba kwa chochote unachokipanda, kwa chochote unachokitoa ni lazima ukivune.

Kama hiyo iko hivyo, ni muhimu sana kwako kutambua mchago wa maneno, vitendo, maamuzi na chaguzi tunazozifanya kila siku kwenye maisha yetu. Hayo yote kwa mujibu wa sheria hii ni rahisi kuturudia kama vile tulivyotoa.
Kwa hiyo kwa chochote kile unachokifanya leo, elewa kabisa unapanda mbegu ambayo utavuna kesho. Kama hutaki matokeo mabaya na kupata kile ambacho hukipendi, jifunze kufanya leo yaliyobora sana na ya manufaa.
Hakuna binadamu ambaye yupo chini ya jua, anaweza kukwepa matokeo ya sheria ya 'karma.' Uwe unajua au hujui sheria hii matokeo ni lazima uyapate, kulingana na kile ulichokipanda siku za nyuma.
Kanuni au sheria hii, inatufundisha na kutumbukusha mambo kadhaa kama ifuatavyo;-
1. Chochote unachopanda kwenye hii dunia ni lazima utakivuna.
2. Maisha yako hapo hivyo si kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya mchango wako kwa mambo fulani uliyowahi kuyatoa kipindi cha nyuma.
3. Kwa mabadiliko yote unayoyataka, ni muhimu kuanza kubadilika wewe. Usipobadilika wewe hakuna ambacho unaweza kukifanikisha kwenye maisha yako.
4. Chochote kile ambacho kinakwenda hovyo kwenye maisha yako, chanzo kikubwa ni wewe. Hapa sheria ya 'karma' inatutaka kuwajibika kwa miasha yetu kwa asilima zote.
5. Unapata au kufanikiwa kwenye maisha yako kwa kile ambacho umekifanyia kazi au ambacho unakifanyia kazi katika maisha yako.
Kwa kujiua sheria hii 'karma,' ni vyema ukawa makini na kile unachofanya kila wakati, maana kitu hicho ni lazima kikuletee matunda yako, hata kama si leo utavuna hata siku nyingine.
Kumbuka sisi ni matokeo ya yale tunayo yafanya kila siku. Hakuna mtu ambaye amekuonea kwa hicho unachokipata na wala hakijaja kwa bahati mbaya au nzuri, bali chanzo chake ni wewe.
Endelea kujifunza kuptia DIRA YA MAFANIKIO kila siku, tukutane wiki ijayo kuweza kuangalia aina nyingine ya sheria ya asili ya mafanikio ambayo  itabadilisha maisha yako.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.