google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 23, 2018

Wewe Ni Mtawala Na Mfalme Wa Maisha Yako Kwa Namna Hii.

No comments :
Kila unapoanza siku yako mpya, naomba uweke akilini hili na kutambua kwamba wewe ndiye unayatawala maisha yako kwa kila kitu. Hakuna ambacho wewe si chanzo cha kutawala. Wewe ndio unatawala na kuamua maisha yako yawe ya mafanikio au kushindwa.
Nikiongea kwa mifano, angalia, wewe unatawala matendo yako. Hakuna mtu ambaye anaweza akakuongoza, wewe ndiye unayeamua uchukue hatua hii au usiichukue kabisa na uachane nayo ufate mambo mengine.
Wewe ndiye unatawala akili yako. Hakuna anayeweza kukuamulia usome kitu fulani au uache. Hakuna anayekuamulia uangalie tv au usiangalie. Wewe ndiye mtawala wa akili yako na akili hiyo inakuongoza kufanya yale uyatakayo.
Wewe ndiye unatawala mtazamo wako. Kwa mtazamo wako ulionao, wewe ndio unaruhusu sana uwe na mtazamo wa namna hiyo. Hakuna mtu ambaye anakuamuru uwe na mtazamo wa aina fulani kama si wewe, mtazamo wako unabebwa na wewe.

Wewe ndiye unatawala mwili wako, hakuna anayekuamulia ule nini au usile nini, hakuna anayekuamulia ufanye zoezi la aina fulani au usifanye, hakuna anayekuamulia uamke mapema au usiamke, mwili wako unautawala wewe na kwa kila kitu.
Wewe ni mtawala wa mahusiano yako, mahusiano hayo yanaweza yakawa ya kimapenzi au ya kawaida. Hakuna anayekuzuia kuwa na mahusiano na watu wengine. Uchaguzi wa nani ujenge mahusiano naye nae, unabaki nao wewe binafsi.
Wewe ni mtawala wa muda wako. Ni wewe ndio ambaye kila wakati unaamua muda wako uutumie zaidi kwenye jambo gani. Pengine uutumie muda wako kwenye jambo linalokupa mafanikio au uutumie kwenye jambo ambalo linakupa hasara.
Wewe ndio mtawala wa hisia zako. Tunaona hisia kama wasiwasi au woga ni wewe ambaye unaamua kuzibeba au kuzipoteza lakini wewe ni mtawala wa hayo mambo tena kwa kiasi kikubwa sana na unatakiwa uelewe hivyo.
Wewe ni mtawala wa matokeo ya maisha yako. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako, chanzo kikubwa ni wewe. Kwa hiyo hutakiwi kulaumu kitu, utawala huo unao wewe na unatakiwa kuelewa hili kwa ufasaha na kufanyia kazi.
Ukiangalia kwa makini utagunduia wewe ni mtawala wa kila kitu kwenye maisha yako. kama iko hivyo kwa nini ulaumu wengine wamekuharibia maisha yako.  Tambua ni sehemu ndogo sana ambayo imechangia hao waharibiu maisha yako kama unavyofikiri.
Kuanzaia leo elewa wewe ni mtawala wa maisha yako na kama iko hivyo kwako, unatakiwa kukubali kuwajibika kwa sababu wewe ni mtawala wa maisha yako na chochote kinachokutokea kwenye maisha yako kinakuhusu haswa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia  wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.