google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 9, 2018

Hili Ndilo Darasa La Kudumu La Mafanikio Yako Wakati Wote.

No comments :
Maisha yana kitu cha kukufundisha leo, kitu hicho kinaweza kuwa kizuri kwako au kitu kibaya kwako ambacho hata kinakuumiza lakini kipo kitu cha kukufundisha kwenye maisha yako ambacho unatakiwa ukifanyie kazi.
Kila mtu unayekutana leo ana kitu cha kukufundisha wewe. Haijalishi mtu huyo amekupa hasira au amekufanya kitu gani, lakini kipo kitu cha kujifunza kwa mtu ambaye unakutana naye, pasipo kujali umri wake au nini alichonacho
Pia kila hali unayokutana nayo leo kwenye maisha yako, hali hiyo ina kitu muhimu cha kukufundisha. Hata kama unapitia kwenye hali ngumu au hali nzuri lakini hali hiyo ina kitu cha kukufundisha na kukufanya uwe imara kimaisha.
Maisha yatakuwa ya maana kwako sana kama utakubali kujifunza kwa kila unachokutana nacho kwenye maisha yako. Ukikubali kujifunza utakuwa katika busara na pia itakuwa ni rahisi kuweza kukabiliana na kila magumu unayokutana nayo.

Wengi wanaona maisha hayaeleweki au maisha hayana maana, hiyo yote ni kwa sababu ya kukaza shingo zao na kukataa kujifunza kutokana na maisha yanavyokwenda. Maisha peke yake yalivyo unatakiwa kujua kwamba ni shule tosha.
Sasa kama unasubiri mpaka uandikiwe ‘notisi’ ndio uelewe kile ambacho maisha yanataka kwako, hapo ndipo unapojikuta unajiangusha wewe. Unatakiwa kila hali, tukio na kila mtu unayekutana naye ukubali kujifunza kupitia yeye.
Kwa hiyo iwe katika magumu, katika hali za kukatisha tamaa au katika mazuri yoyote unayokutana nayo maisha yanakupa kitu cha kukufundisha. Hata kama huna kitabu kupitia mazingira na matukio, kuna kitu unatakiwa ujifunze juu ya maisha yako.
Chagua kujifunza kitu kila siku katika maisha yako, changua kuisikiliza dunia inasema nini juu ya wewe. Usiishi tu kwa mazoea kwa kuishi kama vile wewe utakavyo au uwazavyo. Tambua kabisa kila siku unayokutana nayo ina kitu cha kukufundisha.
Usiwe miongoni mwa watu ambao wanashindwa kwa sababu ya kugoma kujifunza. Kila siku ifanye liwe darasa kwako la kujifunza kitu kipya juu ya maisha yako. Ukifanya hivyo baada ya muda utakuwa mbali sana kwani kila wakati utakua unabadilika na kukua kimafanikio.
Sehemu sahihi na darasa sahihi la mafanikio wakati wote ni kwa wewe kuamua kujifunza kila siku kutokana na chochote unachokutana nacho. Ukiamua kujifunza kweli kuna kitu vitu vingi utavikipata na utafanikiwa  kwa kiasi kikubwa.
Je, jiulize upo tayari kukaa kwenye darasa la mafanikio la kudumu kwenye maisha yako na ambalo litakupa mafanikio? Kama jibu ni ndiyo endelea kujifunza kila siku kutokana na kile ambacho unakutana nacho kwenye maisha iwe ni watu, mazingira au chochote kile.
Hebu leo fanyia kazi darasa hili la kudumu la mafanikio na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.