google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 16, 2018

Ukiwa Na Tabia Hii Moja Tu, Itakuzuia Sana Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Zipo tabia nyingi ambazo zina mchango mkubwa sana kwa anguko la maisha ya wengi. Na kwa bahati mbaya, wengi wanakuwa hawajui kama tabia hizo ndizo zinazowaangusha na hivyo hujikuta ni watu wa kurudia tabia zile zile kila wakati.
Matokeo yake ya kutokujua tabia hizo, hupelekea wengi kuanguka kweli na kunakuwa hakuna mafanikio yanayoonekana na mwisho watu hawa hujiuliza sana ni kitu gani kilichotokea hadi maisha yao yakawa katika hali hiyo.
Leo kwa kupitia makala haya tutajiffunza tabia moja tu ambayo kama ukiwa nayo itakukwamisha sana kwenye safari yako ya mafanikio. Nasema hivyo kwa sababu, kuna watu tayari wanayo matokeo mabovu yamewapata sababu ya tabia hizo.
Tabia moja ambayo itakukwamisha sana na haitakusaidia kufanikiwa kama utakuwa nayo na kuiendeleza ni ile tabia ya kuamua kuwa mtu wa kushangaa katika maisha. Wapo watu ambao tabia zao ni kushangaa tu karibu kitu.

Kwa mfano, Utakuta wao ni watu wa kushangaa na kuhamasika sana na miradi wanayofanya watu wengine, ukija upande wao hakuna hata kitu kimoja wanachofanya au hawachukui hatua kabisa.
Pia utakuta ni watu wa kuingia kundi moja, wanashangaa kinachoendelea humo na kutoka na kuingia tena kundi lingine wanashangaa wee na kutoka tena, pia bila kuchukua hatua. Watu wenye tabia za namna hii kamwe ni watu wasiofanikiwa.
Dunia ya sasa hivi ni ya mwendo kasi, watoto wa mtaani wanakwambia hutakiwi kuuza sura’, fanya kazi. Kama kuna fursa hata kama ni ndogo, itumie ikusaidie kufanikiwa na acha kubaki tu kuwa mtu wa kushangaa.  Kama ni kujifunza, jifunze kweli.
Uzuri au ubaya wa maisha hakuna ubabaishaji, ukileta ubabaishaji wa aina yoyote ile, utaumbuka tu na ni lazima utajibiwa na maisha kama vile wewe unavyobabaisha. Badilika rafiki na achana na biashara ya kushangaa, kuwa mtendaji na aamua kufanya kazi.
Jiulize utashangaa hadi mwaka gani au hadi lini. Watu wanaoshangaa ni mara nyingi ni watu ambao hawafanikiwi. Maisha yanataka uwe mtendaji zaidi na si kuishia kushangaa ambako haukuwezi kukusaidia chochote.
Kama ulikuwa una tabia ya kushangaa basi ndoto na mipango yako mingi sana itaweza kukwama na hautaweza kufanikiwa. Wale wote wanaofanikiwa hawashangai bali wanaamua kujifunza na kuamua kuchukua hatua za kusonga mbele.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.