google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 21, 2018

Fanyia Kazi Mambo Haya 4, Yataleta Mabadiliko Na Mapinduzi Makubwa Ya Maisha Yako.

No comments :
Hakuna muujiza wala ramli  katika kufikia mafanikio yako.  Mafanikio yanajengwa juu ya kanuni tena wakati mwingine kanuni hizo zinakuwa ndogo ndogo sana ambapo wakati mwingine  zinapuuzwa lakini ndizo zijengazo mafanikio yako na ya mwingine.
Hakuna siri tena, ukifanyia kazi mambo ya msingi katika mafanikio utafanikiwa moja kwa moja. Ukumbuke, Yapo mambo mengi ya kufanyia kazi, lakini hapa kupitia makala haya nakupa mambo manne tu, kama ukiyafanyia kazi yataleta mapinduzi ya maisha yako.
1. Tambua ulipo sasa kimaisha na wapi unapokwenda.
Kitendo cha kujua hapo ulipo kimaisha ni hatua nzuri ya kukufanya uchukue hatua za ziada. Ila unatakiwa ujue, kujua hapo ulipo haitoshi, unatakiwa kujua ni wapi unakwenda kimaisha baada ya miaka miwili au baada ya miaka mitano.
Ukijua pale ulipo pengine upo kwenye hali mbaya sana, lakini na ikawa haujui ni wapi unakwenda kwenye maisha yako nalo hilo ni tatizo kwako. Kama hujui unakokwenda ni dalili tosha inaonyesha hautafanikiwa maana utafanya chochote ilimradi iwe hivyo.
 2. Tambua ndoto yako ni ipi.
Jiulize hapo ulipo una ndoto ya maisha yako. Je, una kitu ambacho unataka kukitimiza na tayari umeshaanza kukichukulia hatua. Kama huna ndoto yoyote ya kimaisha niseme kwa uwazi kwako hutaweza kufanikiwa.
Kutaka kuishi maisha ya kimafanikio halafu huku ukiwa mweupe, ukiulizwa kile unachokitaka kila kitu unajisemea na unakitaka huko ndiko kunaitwa kupotea. Ni lazima ndoto yako iwe wazi, hata ukiulizwa usiku wa maneno ndoto yako ni ipi, unaisema tu.
 3. Tambua ni kipi utakifanya ili kutimiza ndoto zako.
Kujua ndoto yako peke yake haiwezi kukupa uhakika wa kufanikiwa, unatakiwa ujue pia ni kipi utakifanya ili ndoto zako zitimie. Hapa ni lazima ujue kazi au shughuli ambayo utaifanya karibu kila siku ili ikusaidia kukusogeza kwenye ndoto zako. 
Ukishajua ni kipi ambacho unatakiwa kukifanya ili kuhakikisha ndoto yako inatimia, hapo ndipo kitu hicho unatakiwa kukifatilia kila siku. Tafsiri yake ni hii, kushindwa kufanya kitu hicho unajiweka kwenye wakati wa kukwamisha ndoto yako.
 4. Chukua hatua mapema.
Asikudanganye mtu mafanikio yako hayaji kwa mdomo tu au kwa kusema. Mafanikio yako yanakuja kwa wewe kuchukua hatua tena hatua za kuweza kukusaidia kufanikiwa. Ukichukua hatua utaweza kufanikiwa tena kwa kiasi kikubwa tu.
Ikiwa utaendelea kusema tu kila wakati bila kutekeleza ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwako. Kuchukua hatua mapema ndio mpango mzima na sahihi wa kukuwezesha wewe kufanikiwa kwa kile ukifanyacho.
Fanyia kazi mambo hayo kila siku na uwe na uhakika utaleta mabadiliko ya maisha yako kila unapofanyia kazi mambo hayo, tena mabadiliko hayo utayaleta kwa kiasi kikubwa sana mpaka unaweza ukafika wakati ukashangaa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,



                                                       


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.