google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 5, 2018

Unaharibu Au Kutengeneza Maisha Yako Kwa Sababu Ya Kuruhusu Mambo Haya.

No comments :
Kwa chochote unachokiruhusu kikurudishe nyuma kwenye maisha yako kitu hicho kitakurudisha nyuma na kwa chochote unachokiruhusu kikupeleke mbele kwenye maisha yako basi kitakupeleka mbele hadi kwenye mafanikio yako.
Kwa mfano, kama umeruhusu changamoto unazopitia ndizo ziwe chanzo cha kukurudisha nyuma basi uwe na uhakika utarudi nyuma, na kama pia umeruhusu changamoto zako ziwe ndio chanzo cha kuweza kukufanikisha basi ujue utafanikiwa.
Kufanikiwa kwako kunategemea sana, ni nini ambacho unakiruhusu kikutokee. Wewe ndie chanzo kikubwa cha mafanikio yako. Unatakiwa uwe makini na ujue hasa ni kitu kipi au mambo gani ambayo unaruhusu kwenye maisha yako yawe chanzo cha kufanikiwa kwako au kushindwa.

Yapo mambo ambayo ukiyaruhusu kwenye maisha yako yanakupa mafanikio na yapo mambo ambayo ukiyaruhusu kwenye maisha yako yanakufungulia njia ya kuweza kushindwa, hapa ndipo unatakiwa ujue jinsi ya kutambua.
Unapaswa kujua zipo sababu na hali tofauti zinazofanya maisha yako yawe kama hivyo yalivyo, lakini  hiyo yote inatokana na jinsi wewe unavyoruhusu baadhi ya mambo kwenye maisha yako. Inategemea unaruhusu nini kikusogeze mbele au nini kikurudishe nyuma?
Ni wazi hakuna anayependa kurudi nyuma kwenye maisha yake, lakini ni ukweli kwamba yapo mambo ambayo ukiyaruhusu ni lazima yatakurudisha nyuma sana kwenye mafanikio yako hata kama hupendi na yapo mambo ukiyaruhusu yatakupeleka mbele tu.
Huwezi ukafanikiwa kama unaruhusu uzembe, hujitumi au unakosa nidhamu binafsi. Kwa kuruhusu mambo hayo utakwama lazima na kinyume chake kama unaruhusu kujituma, kujifunza kukazana kwa kile unachokifanya pia utafanikiwa.
Maisha yako hayo uliyonayo hujayapata kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya yale mambo ambayo umeyaruhusu kwenye maisha yako na ndio ambayo yameumba maisha yako yawe hivyo yalivyo leo hii.
Huwezi hata kidogo kukwepa kwamba wewe ndio chanzo pekee cha maisha yako na wewe ndie chanzo cha uliyefanya maisha yako yawe hivyo yalivyo, ni lazima ujue unawajibika kwa namna yoyote ile kutengeneza maisha yako.
Kaa chini na tafakari kwa kujiuliza ni mambo gani ambayo uliyaruhusu na unaruhusu sasa ambayo yamekuwa chanzo cha kuharibu au kutengeneza maisha yako, ukishayajua mambo hayo kuwa makini nayo.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.