google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 6, 2018

Ukiijua Thamani Ya Siku Yako Ya Leo…Utabadilisha Maisha Yako Hivi.

No comments :
Leo upo kwenye siku mpya, siku ambayo hujawahi kuigusa, hebu naomba ifikirie siku ya leo ambayo unayo, kisha jiulize ni kItu gani cha thamani ambacho utakwenda kukifanya katika siku ya leo na ili kikuachie kumbukumbu ya kudumu?
Zipo fursa na mambo  mengi mazuri kwako ambayo unatakiwa uyafanye leo hii ili iwe siku yako ya faida na kila ukikumbuka useme ndiyo, kuna wakati  nilifanya kitu ambacho kinanisaidia sana kwenye maisha yangu.   
Unaweza ukachagua wewe mwenyewe kitu cha aina fulani ambacho kitakufanya usonge mbele kwenye maisha yako, au unaweza ukachagua kitu fulani kitakachokurudisha nyuma kwenye maisha yako, wote huo bado ni uamuzi wako.
Unaweza ukachagua kuwasaidaia wengine ili kuifanya dunia kuwa sehemu ya amani na salama zaidi au unaweza ukachagua kuendelea kuwadidimiza wengine pia hilo nalo wewe unachagua, ni kipi ambacho kwako unatakiwa ukifanye.

Yapo mambo makubwa ambayo unaweza ukaamua kujifunza na kuyafanyia kazi leo, ambapo baadae yatabadilisha sana maisha yako. Na yapo pia mambo ambayo unaweza ukaamua usijifunze na kuyafanyia kazi yoyote ile.
Ipo thamani kubwa sana katika siku ya leo, ikiwa utaamua kuzitumia fursa za siku ya leo kwa uhakika mkubwa na ukumbuke itapita siku na miaka mingi utaikumbuka sana siku ya leo, kama kweli utaamua kuitendea haki katika kutengeneza maisha yako.
Hapo ulipo ndipo unatakiwa kuanzia, haijalishi una pesa mfukoni au huna, ila tengeneza thamani, ambayo itafanya siku yako ya leo iwe ya kukumbukwa wakati wote kama si wewe, basi hata na kizazi chako kijacho.
Thamani na fursa ambazo utaamua kuzitumia leo, hazitaishia hapa tu, bali thamani hiyo itazidi kuendelea na kuenea kadri siku na miaka mingi itakavyokwenda. Matunda ya ulichowekeza leo yataonekana pasipo kujali itapita miaka mingapi.
Unatakiwa kuweka akilini kwamba, kwa fursa yoyote utakayoitumia vizuri katika siku ya leo, itakuwa ni ya kukumbukwa na itaifanya siku hii ya leo kuwa  ni siku ya faida kubwa sana kwako wakati wote wa maisha yako.
Usikubali kuipoteza siku yako kwa kufanya mambo ya kizembe hata kidogo, fanya mambo ambayo yataifanya kila siku unayokutana nayo ionekane kwamba ilikuwa ni siku ya faida. Usiishi kihasara, ishi kwa kuongeza kitu kila siku.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.