google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 8, 2018

Chanzo Kikubwa Cha Watu Wengi Kushindwa Kwenye Maisha Kinaanzia Hapa.

No comments :
Kufanikiwa kwenye maisha, kunategemea sana kwanza wewe ujue unaenda wapi kwenye mafanikio yako. Kama hujui ni wapi unakoenda kwenye mafanikio yako ni ngumu sana kuweza kufanikiwa. Ni lazima ujue ni wapi unakoenda ili kupata mafanikio uyatakayo. Je, jiulize unajua kule unakotaka kwenda kimafanikio?
Kama unafikiri natania, mtafute mtu yeyote ambaye amefanikisha jambo fulani, ukimwangalia mtu huyo utagundua alikuwa ana mpango au alikuwa anajua kule anakotaka kwenda kikamilifu. Na pia watu wanaoshindwa, kiukweli wengi hawajui kisawa sawa malengo na mipango yao kwa kule wanakotaka kufika kimafanikio.
Watu hawa wanaoshindwa utakuta ni watu ambao wapowapo tu, wanaamka, wanafanya kazi, lakini ukiwauliza nini malengo yao baada ya miaka mitano kuanzia leo hawajui. Kwa mwendo kama huo wa maisha ni ngumu kufika mbali kimafanikio, ndio maana mtu anayejua kule anakoenda ni rahisi sana kuweza kufanikiwa.

Kwa hiyo mpaka hapo unaona kipimo pekee ambacho hata wewe unaweza kukitumia kujua kama kwa baadae utaweza kufanikiwa au hautaweza kufanikiwa ni kwa wewe kujiuliza swali hili mara kwa mara je, ni wapi unapoenda kimafanikio. Kama hujui unakokwenda kimafanikio na mbele yako unaona kama giza, itakuwa ni ngumu kufanikiwa.
Unatakiwa ujue kule uendako kimafanikio kwa uwazi, kwamba pamoja na kwamba mimi nafanya kitu hiki kidogo ambacho hata watu wengi wananicheka, lakini nataka mwisho wangu uwe pale, usiishie kuota tu, baada ya hapo chukua hatua hata kama hatua hizo ni kidogo sana, lakini chukua hatua.
Unapochukua hatua na huku ukiwa unajua kwenye akili yako ni wapi unakoenda, utajikuta unasogea na kuvuta fursa zingine ambazo hukutarajia kuzivuta. Kupoteza mwelekeo wakati unatafuta mafanikio ni jambo la hatari sana kwako. Hutakiwi kupoteza mwelekeo ila unatakiwa kujua kule unakokwenda kila wakati ili usipotee.
Chanzo kikubwa cha watu wengi kushindwa kwenye maisha kinaanzia na wengi kutokujua ni wapi wanakokwenda. Kwa kutokujua wapi unapokwenda unajikuta huna lengo maalumu la kukusaidia kufanikiwa. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na lengo maalumu katika maisha unapoanzia.
Kitu ambacho nataka uelewe hapa ni hiki, ili kufanikiwa tambua kule unakotaka kwenda kimafanikio. Njia ya mafanikio yako unatakiwa uijue kwa uwazi ni wapi unatakiwa uwepo pasipo kujali unakutana na changamoto zipi. Kama utashindwa kujua kule uendako, ujue ndio kushindwa kwako huko kunapoanzia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713048 035,



No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.