google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 15, 2018

Njia Sahihi Ya Kupima Kama Unapiga Hatua Za Kimafanikio Au Upo Palepale.

No comments :
Hapo ulipo unao uwezo wa kupima kama unapiga hatua au hupigi hatua kwa kile ambacho ukifanyacho. Ni rahisi sana kuanza kujiuliza hivi kwa hiki nikifanyacho mimi, napiga hatua au nimebaki pale pale nilipo tu.
Mara nyingi ipo njia sahihi ambayo inaweza ikakusaidia wewe na mtu yeyote kujua kama anapiga hatua ama hapigi hatua. Njia hii si nyingine bali ni kwa wewe kukaa nje ya mazoea uliyoyazoea kila siku.
Ukiona kila siku unafanya kitu hicho kwa namna hiyo hiyo yaani hubadilishi kitu na upo kwenye mazoea yale yale si rahisi sana wewe kuweza kupiga hatua. Kama ukiona kile unachokifanya na unakifanya nje ya mazoea ujue kuna kupiga hatua hapo.
Upo uwezekano wa wewe ukawa bado hujanielewa kwa namna fulani hivi, lakini nitakupa mifano zaidi ambayo itakusaidia kuweza kuelewa. Tambua hivi, ni jambo la hatari kufanya mambo yako kwa hali ya mazoea kila siku, maana hutafanikiwa.
Niweke labda wazi kwako nakurudia hivi, hutaweza kufanikiwa kama hauko nje ya mazoea yako. Mazoea ni moja ya sumu kubwa sana inayokuzuia kufanikiwa. Ukiendelea kufanya mambo yako na mazoea utashangaa unabaki palepale miaka nenda rudi.

Wanaobadilisha maisha ni wale watu ambao wanaamua kwenda nje ya mazoea yao. Kwa tafsiri ya haraka mazoea uliyonayo ndio yaliyokupa matokea uliyonayo. Hivyo kwa kuendelea kuyang’angania utaendelea kupata matokeo yaleyale.
Hiyo inamanisha kwamba, hata kama una malengo na mipango mizuri vipi, ila kama unachukua hatua kwa mazoea, basi utaendelea kubaki pale pale karibu kila wakati kwenye maisha yako na hautaona ukipiga hatua mbele ya kukusaidia kufanikiwa.
Hivyo, kila wakati jaribu kufanya jambo jipya ambalo litakupa matokeo tofauti na yale ambayo umekuwa ukiyapata. Kwa kufanya kwako jambo jipya kuna vitu vingi sana ambavyo utajifunza na vitakubadilishia mtazamo wako kabisa.
Huhitaji kusubiri kitu, anza kujua kama unafanikiwa au hufanikiwa kwa kujipa changamoto ya kukaa nje ya mazoea yako. Hata kama kwako unaona inakuwa ngumu lakini dhamiria kukaa nje ya mazoea uliyonayo kila wakati.
Unapaswa kujua, kitakuwa ni kupimo sahihi kwako kama unapiga hatua au hupigi  hatua za kimafanikio kwa kukaa nje ya mazoea yako. Ukiona unafanya mambo yako na unaona kawaida ujue hakuna ulichobadili na hapo kufanikiwa itakuwa shida pia.
Jitahidi uwezavyo kama nilivyosema kaa nje ya mazoea yako, hiyo itakusaidia kukujengea nidhamua na hata kukupa mafanikio ambayo hukuyatarajia kwa sababu ya nidhamu yako. Hivi ndivyo unavyoweza kupima mwendelezo wa mafanikio yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.