google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 10, 2018

Kama Una Moyo Huu…Unatengeneza Mazingira Sahihi Ya Kufanikiwa.

No comments :
Kila wakati unapokuwa na moyo wa shukrani kwa jambo lolote lile, tambua unakua unajiweka kwenye dunia ya mafanikio moja kwa moja hata pengine pasipo wewe kujua. Nikiwa na maana yaani unakuwa unajiweka kwenye ulimwengu wa watu wanaofanikiwa.
Kitu chochote pia ambacho unakua unakitolea shukrani iwe maisha au kitu chochote ambacho umekipata, ukichukua tu ile hatua ya kushukuru kwa kitu hicho ujue kabisa kitu hicho kinaongezeka thamani tofauti na ambavyo usingeshukuru.
Kwa mfano, kama umepata mtaji wa shilingi laki tano , na ukaamua kushukuru kwamba umepata mtaji huo ujue kabisa kuna thamani kubwa ambayo inaongezeka kutokana na mtaji huo ambao unakuwa umeupata.
Tambua kila unapoamua kuwa na moyo wa shukrani, hiyo inakufungulia uwezo wa mambo mengi  ikiwa pamoja na uwezo wa kuona fursa ambazo ulikuwa huzioni kwenye maisha yako kabisa kabla ya hapo.
Unapokua na moyo wa shukrani na ukaruhusu moyo wako ukatamka maneno ya shukrani, elewa shukrani hiyo inafungua milango ambayo hukutakiwa kuiona milango hiyo mpaka uwe na shukrani ambayo umeitoa.
Kwenye maisha yako zipo baraka na maisha ya mafanikio  makubwa yanakusubiri mpaka uanze kuwa na shukrani. Moyo wa shukrani pekee ndio unaweza kukusaidia kufungua milango mingi ya mafanikio kwako.
Utakuwa ni mtu wa kujifungia baraka sana, kama utaendelea kutokuwa na moyo wa shukrani. Kama ukianza kuwa na moyo wa shukrani utashangaa kuanza kuona mambo mengi yakibadilika kwenye maisha yako.
Angalia mifano kwenye kwenye maandiko matakatifu ni kitu gani ambacho kiliwatokea watu ambao walikuwa na shukrani, utaona bila shaka ni mafanikio makubwa yaliwatokea na hicho ndicho kitu unatakiwa kukijua.
Unapochagua kuishi maisha ya shukrani maanake unakuwa ni mtu ambaye umechagua kuishi maisha ya mafanikio kiroho hata kabala hujafanikiwa kwa nje. Wakati wote mafaniko yanaanzia ndani yako na si nje.
Kuanzia leo anza kuwa na moyo wa shukrani kwa mambo mengi katika maisha yako. usiwe mtu ambae hauna shukrani. Hebu anza kuwa na shukrani kwa kile unachokipata, kuwa na shukrani kwa Mungu na kuwa shukrani na kwa wengine pia.
Unapojijengea moyo wa kushukuru kwa namna hiyo, itakusaidfia sana kuweza kubadili 
maisha yako. Kama unafikiri natania, anza leo kuwa na moyo wa shukrani na kisha uone jinsi ambavyo maisha yako yatabadilika.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.