google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 22, 2018

Hivi Ndivyo Watu Wanavyopenda Kushindwa Kwenye Maisha.

No comments :

Unaweza ukaona kama ni kitu cha ajabu au kama nimekosea vile kuandika kichwa cha habari ya makala haya, lakini elewa sijakosea na ninachokimaanisha ndicho, lipo kundi kubwa la watu linapenda kushindwa kwenye maisha.
Unashangaa, ndio, kundi hili kubwa ndilo ambalo likiulizwa, lina mipango mizuri sana ya kimafanikio, lakini maneno na vitendo vya kutaka maisha hayo haviko sawa. Kundi hili kubwa ambalo labda na wewe upo, hujikuta likipenda kushindwa kufanikiwa maishani.
Najua unajiuliza kivipi? Hebu angalia kuna watu ambao muda wao muda mwingi sana ni kuangalia Tv, utakuta zaidi ya saa tatu mtu amekaa anaangalia Tv, unategemea hapa nini kitatokea kama si kuanguka tena vibaya kwenye maisha yake.

Ule muda mwingi unaopotea kwenye kuangalia Tv, naamini ungetumuka kufanya kitu kingine kama kutafuta maarifa ya aina fulani hivi, basi mtu huyo angekuwa yupo mbali sana kimafanikio.  Kwa bahati mbaya muda huo unapotezwa mchana kweupe.
Si Tv tu peke yake, ukiwaangalia watu wengi wanaishi maisha ambayo hayana maana kabisa, ni watu wa kuishi maisha ya kuwadanganya na kuwapoteza kabisa kwa kufanya vitu ambavyo haviwastaili. Ni watu ambao dhahiri wanajidanganya.
Kwa kawaida unapofanya mambo yanayoenda kinyume  na mafanikio, hata kama unatamka mara ngapi kwamba wewe unataka mafanikio hayo, hiyo haitaweza kukusaidia kitu. Ndio maana unatakiwa usijidanganye kwenye maisha yako mwenyewe.
Unatakiwa utafute vitu vya kufanya ambavyo vinakusaidia kukupa mafanikio. Hata hivyo kwa bahati mbaya unaishi maisha ambayo kiuhalisia kwa maisha hayo hayakusogezi mbele hata kidogo kuweza kufanikiwa sana sana yanakurudisha nyuma.
Watu wengi inaonyesha wanajishughulisha na kazi ndogo ndogo ambazo haziwasaidii kupiga hatua. Kazi hizo zinaweza zikawa kama kupiga stori, kudhurura na kufatilia habari zizsizo na maana. Mafanikio hayawezi kuja kwa namna hiyo hata siku moja.
Waangalie watu waliofanikiwa, wamefanikiwa kwa sababu ya kuishi na tabia za kimafanikio. Pia waangalie watu ambao wameshindwa nao pia wameshindwa kwa sababu  ya kuishi na tabia zile za kushindwa.
Nimekwambia hata uimbe wimbo mzuri vipi ambao unajisemea kwamba unataka maisha mazuri, ila kama unaishi maisha yanayokurudisha nyuma utakwama tu. Hakuna muujiza katika kukupa mafanikio yako. muujiza ni wewe.
Anza kubadilika ishi tabia za watu wa mafanikio ili ufanikiwe. Ukiendeleza ubishi nakwambia utakwama sana. Amua kujifunza, acha kudharau yale ambayo kuna watu walipoteza muda wao kukusaidia wewe.
Kumbuka matendo yako ya kila siku ambayo unayetenda kinyume na mafanikio ndio yanayotuonyesha kwamba wewe unapenda sasa kushindwa. Hata kama hutaki kama unatenda kinyume na mafanikio, ujue basi unapenda kushindwa kwenye maisha yako.
Ishi kwa kujiamini, amua kusonga mbele kwa kuhakikisha kila unachokifanya, kiwe na matokeo ya kukusogeza wewe mbele. Ukiona kitu hicho kikimbie na hakina maana ya kuweza kukusaidia leo na hata kesho.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia  wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.