google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 20, 2018

HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maneno Mabaya Yana Mwangwi Mkubwa Kuliko Maneno Mazuri.

No comments :
Mbali na kanuni za kimafanikio ambazo tumekuwa tukijifunza mara kwa mara, lakini unapaswa kujua kwamba pia maisha ya mafanikio yametawaliwa sana na hekima. Hiyo yote  inaonyesha hekima ni za msingi sana katika maisha yetu pia.
Hekima zinatufunza busara, hekima zinatufunza namna ambavyo tunatakiwa kuishi na jamii inayotuzunguka na hekima pia zinatusaidia kuweza kujifunza kanuni kwa ujumla za mafanikio zilizopo kwenye maisha yetu.
Kwa mantiki hiyo, katika siku hii ya leo, nikukaribishe, tuweze kujifunza kwa pamoja baadhi ya hekima za maisha na mafanikio. Ni kusudio langu utatoka na kitu cha kuweza kukusaidia na ambacho utakifanyia kazi.


1.  Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.
Katika hekima hii inatuonyesha katika maisha, unaweza ukamfanyia mtu kitu ambacho kitagusa maisha yake pasipo kujali kitu hicho ni kibaya au kizuri, lakini kumbukumbu inakuwa inabaki sana kwa yule aliyeguswa na alichofanyiwa.
Ndio maana unaweza ukamsaidia mtu usikumbuke, unaweza ukamfanyia mtu ubaya usikumbuke, lakini yule aliyefanyiwa ubaya huo anakuwa anakumbuka sana. Hapa ukumbuke  tunaaswa kuwa makini  yale yanayogusa maisha ya wengine.
Jiulize ni mara ngapi au kuna wakati uliwahi kumfanyia mtu kitu fulani ambacho kilimsaidia, utakuta muda unakuwa umepita na wakati huo umesahau, lakini unapokutana na mtu yule anakukumbusha na kukwambia unakumbuka ulinifanyia kitu hiki.
Mara nyingi wengi wetu hubaki tukishangaa kwa kukumbushwa kitu kile. Kwa hiyo unaona hata ubaya ukimfanyia mtu ni hivyo hivyo. Kwa wewe ukiyefanya ni rahisi kusahau lakini si kwa ,mtu aliyefanyiwa ubaya huo hata kidogo hawezi sahau.
Hapa ndipo unaweza ukapata picha kwa nini shoka halikumbuki mti liloukata na kwa nini mti uliokatwa hulikumbuka shoka. Unaona mti unakumbuka shoka kwa sababu shoka liligusa maisha ya mti huo kwa namna fulani.
2. Maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri.
Ni kawaida sana maneno mabaya kuweza kuenea kwa haraka kuliko maneno mazuri. Unaweza ukafanya mengi mazuri lakini ukikosea kidogo maneno hayo yatasambaa sana kuliko ambavyo hukutarajia iwe hivyo.
Hapa kupitia hekima hii inatunaonyesha wazi kwamba maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri,  hilo ni la ukweli na halina ubishi. Mwangwi wa kitu kibaya unasikika zaidi kuliko mwangwi wa kitu kizuri.
Angalia kipindi ambacho ulifanya ubaya, mwangwi wake ulisikika vipi na kipindi ambacho ulipofanya mazuri mwangwi wake ulisikikaje pia. Hapo utagundua kipindi ambacho ulifanya mabaya mwangwi wake ulionea sana.
Tahadhari kubwa unayopewa hapa ni kuwa makini sana na maneno mabaya. Kwa tafsiri nyingine inaonyesha tenda wema unavyoweza wewe ila uelewe maneno mabaya siku yakija kukuibukia yana mwangi sana kuliko maneno mazuri.
Fanyia kazi hekima hizi naamini kwa sehemu zitakuwa zimekusaidia kutoka hatua moja na kulekea hatua nyingine ya maisha yako. Kila wakati hekima zinakupa busara, hekima zinakuza uelewa wako kwa namna fulani.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama pia  wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.