google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 7, 2018

Hatua mbili Za Kufuata Ili Kufanya Kile Unachokiandika Kibaki Na Maana Siku Zote.

No comments :
Inabidi ufike mahali ukubali na uamue kwamba kile unachokiandika kiwasaidie wengine na kugusa maisha ya wengine kwa asilimia kubwa.  Haitakuwa na maana kama una andika tu, halafu kupitia uandishi wako huo hakuna ambacho kinabadili maisha ya wengine.
Kupitia somo hili, nataka nikuonyeshe jinsi unavyoweza kuwa mwandishi bora, ikiwa utafuata hatua hizi, kama nilivyozielezea kwa kifupi . Nategemea kwa kuwa pamoja nami hadi mwisho utajifunza kitu cha maana.
1. Andika kile ambacho kinagusa maisha ya watu.
Kama nilivyosema, unapoandika jambo lolote, hakikisha jambo hilo linagusa maisha ya watu wengine. Usiandike ilimradi umeamua kuandika, andika ukiwa na uhakika hiki ambacho unakwenda kukiandika kinakwenda kubadilisha maisha ya mtu fulani na sehemu fulani.
Nikwambie hivi labda, kazi zako zitabaki kuwa hazina maana kama utaendelea kuandika vitu, ilimradi tu umeandika. Gusa maisha ya watu, pengine unajiuliza kile ninachokiandika nitajua vipi kama kinagusa maisha ya watu?
Ni rahisi tu, utajua tu kwa kuangalia kwanza wewe kitu hicho kimekugusa au kimekusaidia kwa kiasi gani, kama hakijakusaidia wewe mwandishi na mwingine huko hakiwezi kumsaidia pia. Kwa hiyo jitahidi kuandika kile kinachogusa maisha ya watu.

2. Chagua ni aina gani ya uandishi unaotaka kuutumia.
Hapa inabidi uchague aina ya sauti unayotaka kuitumia kufikisha ujumbe wako. Unatakiwa kutambua tu kila mtu ana namna yake ya kufikisha ujumbe kwa jamii na ndio maana mwandishi mmoja na mwandishi mwingine wanakuwa wanatafautiana.
Hivyo, inabidi ujiulize je, unataka kufikisha ujumbe wako kwa kutumia aina gani ya uandishi. Maana zipo aina tofauti za kufikisha ujumbe wako ama ‘platform’ unayotaka kuitumia kufikisha ujumbe wako. Kwa mfano;-
Uandishi wa kiundishi wa habari/Journalist, hapa kama wewe si mwandikaji mzuri sana, unaweza ukatumia aina hii ya uandishi kwa sababu, unaweza ukatumia njia  kuwauliza watu maswali na maswali yale ukayachapa na kuyatumia kuyaweka katika mtandao kama unaendesha blog.
Uandishi wa kinabii/Prophecy, katika aina hii ya uandishi kama utautumia uandishi huu, kila kitu unachokiongea au kukiandika ndio kinakuwa ukweli wenyewe. Hapa mwandishi unatakiwa uandike ukweli mtupu kuhusu maisha ya watu bila kupepesa macho kutokana na uzoefu wako. Kazi za uandishi wa kuhamasisha mafanikio zipo hapa.
Uandishi wa kisanii/Artist, kazi au uandishi unaokuwa unawasilishwa kwa njia ya kisanii mara nyingi unakuwa unatumia mvuto fulani hivi ili ujumbe kufika. Kwa mfano, uandishi wa mashairi au kuandika kazi kwa kutumia katuni ni mojawapo ya uandishi wa kisanii ambapo kupitia kuchekesha ujumbe unaifikia jamii.
Uandishi wa kitaaluma/professor, kila kitu kinachoandikwa katika aina hii ya uandishi kinakuwa kinaonyeshwa chanzo chake. Uandishi wa namna hii hauendi kama hakuna chanzo cha ulichokiandika kimetoka wapi. Hapa mwandishi hutakiwi kuwa mazoefu tu, bali unatakiwa uwe umesoma vitabu vingi sana ili uvifanyie rejea.
Hapa uamuzi ni wako kuchagua ni aina gani ya uandishi ambao kwako unauona unafaa na kuamua kuutumia. Hata hivyo ingawa waandishi wengi huwa hawajui ni aina gani ya uandishi wanaoutumia katika kazi zao, hujikuta tu wakiandika.
Kwa kufuata hatua hizo uandishi wako utabaki kuwa na maana siku zote na utakuwa na sehemu ya kubadilisha jamii yako siku hadi siku, pia vizazi na vizazi.
Fanyia kazi hatua hizo mbili muhimu na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.