google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 12, 2018

Anza Na Hatua Hii Muhimu Ili Ikusaidie Kufikia Mafanikio Yako.

No comments :
Kama huwezi kuchukua hatua kubwa za kuelekea kwenye malengo yako uliyojiwekea, basi chukua hatua ndogo tu. Kama unashindwa kuchukua hatua ndogo pia, basi ujue hujaamua kujitoa kuweza kufanikisha malengo yako hayo.
Utakuwa ni mtu wa kushindwa sana kama huchukui hata hatua ndogo. Unapochukua hatua ndogo ndogo ukumbuke,  hatua hizo ni muhimu na zinakusogeza sana kukupeleka kwenye malengo yako kila unapozichukua.
Acha kudharau hatua zozote zile ndogo. Anza kuchukua hatua ndogo kwani zinakuwa ni mwanzo wa safari ya mafanikio yako na zinaonyesha kweli umejitoa kuhakikisha ndoto zako zinatimia hata kama upo kwenye changamoto nyingi za kimaisha.

Watu wenye mafanikio makubwa wengi wao hawakuanza na hatua kubwa za kimafanikio kama unavyofikiri. Wengi wao walianzia chini sana na mpaka ilifika wakati walidharauliwa vya kutosha na kutamani kuacha kile wanachokifanya.
Hata hivyo pamoja na kuanza hivyo hawakukata tamaa, kila siku waliamua kuchukua hatua hizo na hatua hizo ziliwapa nguvu ya kuendelea kusogea au kuongeza hatua zingine na hadi kufika mbali kabisa kimafanikio.
Hebu jiulize sasa kama wewe hutaki kuanza na hatua ndogo ni kipi ambacho unakitaka kwako. Ukumbuke, ushindi mkubwa wowote unaanza na kidogokidogo tu. Hili si swala la bahati mbaya bali naweza nikasema ni kama kanuni ya kimafanikio ndivyo ilivyo.
Hata ukiangalia mimea huwa inaanza kidogo kidogo na mwisho wa siku inakuwa ni miti mikubwa sana ambayo hata hukuweza kufikiri kama ingekuwa miti ya namna hiyo, hicho ndicho kitu kinaweza kutokea hata kwako pia.
Pale ulipo anza na kidogo chochote kile ulichonacho na kidogo hicho uwe na uhakika kitakusaidia sana katika kutengeneza kikubwa. Jambo la msingi usiwe na hofu, anza na hapo hapo ulipo na utashangaa jinsi kidogo hicho kinavyoongezeka.
Je, upo tayari sasa kuanza sasa na hatua ndogo hata kama upo kwenye changamoto nyingi za kimafanikio? Hutakiwi kusitasita, nikwambie tu anza sasa kuchukua hatua hizo ndogo, wakati utafika utachukua hatua kubwa za kuweza kukusaidia kufanikiwa.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.